The House of Favourite Newspapers

Ubwabwa na Maharage Vyataka Kutoa Roho Mbosso

MSANII wa muziki wa kizazi kipya aliye chini ya Lebo ya WCB, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso’ amefunua siri yake kwamba alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kula ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku moja ulitaka kumtoa roho kwani alijikuta akivimbiwa kupitiliza.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mbosso alisema kuwa alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana ubwabwa na maharage kupita maelezo, ukipikwa nyumbani kwao alikuwa hachezi mbali na jikoni, mapema anakuwa amesharudi kwenye michezo yake tayari kusubiria mnuso.

 

“Sijui ilikuwa ni uroho au nini, yaani nilikuwa napenda ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku nilivimbiwa sana, ilikuwa kila nikila sishibi, mwisho wa siku ikawa balaa, ikabidi mama achukue mwiko, akanipigapiga nao tumboni, hiyo ndiyo ikawa nafuu yangu, yaani ilikuwa balaa kwani watu walianza kwa kunipepea ikashindikana lakini nili­pata ahueni baada ya mama kunipa tiba hiyo,” alisema Mbosso.

Stori: Neema Adrian

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.