The House of Favourite Newspapers

LIVE UPDATES: Matukio ya Uchaguzi Kinondoni na Siha, ITV Yatakiwa Kuomba Radhi Nec

Mgombea wa ubunge Jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu tayari ameachiwa, ni baada ya kuwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha polisi Magomeni.

Saa 6:00, Asubuhi: Chadema kimedai MGOMBEA Ubunge Kinondoni, Salum Mwalimu (CHADEMA), amesema yupo tayari kuitwa mharifu ama kupelekwa jela yoyote iwapo ataonekana ametenda kosa kutetea kura zake kufuatia baadhi ya mawakala wa chama hicho kuzuiliwa kuingia kwenye vituo kwa kukosa barua ya utambulisho kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Saa 5:00, Asubuhi:

Baadhi ya mawakala katika eneo la Makumbusho Dar es Salaam wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura huku wengine wakiingia kwa kuchelewa, Ambapo Msimamizi wa Uchaguzi wa eneo hilo amesema mawakala hao walizuiliwa kwasababu walikuwa hawana barua za utambulisho.

 

Saa 4:30, Asubuhi: Licha ya zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Siha Kilimanjaro kwenda vizuri, baadhi wananchi wamelalamikia kutoyaona majina yao katika orodha ya wapiga kura,ili kupata haki ya msingi ya kupiga kura.

 

Saa 4:30, Asubuhi:

Baadhi ya mawakala katika eneo la kata ya Tandale Dar es Salaam.wamelalamikia kitendo cha kutolewa nje ya vituo kwa kile walichoambiwa kuwa hawatambuliki, Huku wao wakidai kuwa wanavigezo vyote.

Saa 4:10, Asubuhi: Kamanda wa Polisi Kinondoni ACP. Muliro Jumanne Muliro amesema hali ya usalama katika eneo hilo ni nzuri, hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kupiga kura kwa ni haki yao ya kumchagua kiongozi wanaye mtaka.

 

Saa 4:00, Asubuhi:

Kinondoni: Kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi Mwongozo katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura ni ndogo.

 

Saa 3:15, Asubuhi:

Siha:  Mawakala 67 kati ya 70 wa Chama cha Wananchi (CUF ) wanaosimamia uchaguzi mdogo Jimbo la Siha wametolewa vituoni kwa madai kuwa barua zao za kiapo zimesainiwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo pekee badala ya kusainiwa na hakimu.

 

 

Saa 2:30, Asubuhi: Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM Maulid Mtulia amepiga kura katika kituo cha Friends Corner, Kata ya Ndugumbi nakusema zoezi hilo limekwenda salama. Amesema atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa.

 

 

Saa 2:10, Asubuhi:

Wananchi wameendelea kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Kinondoni katika Eneo la Mwenge Dar es Salaam, ambapo wamesema zoezi hilo linaenda vyema toka vituo vilipofunguliwa asubuhi hii leo.

 

Saa 2:00, Asubuhi:

ZOEZI la upigaji kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani katika baadhi ya maeneo, Tanzania Bara limeanza limeanza rasmi asubuhi hii ya leo tarehe Februari 17, 2018 ambapo majimbo mawili ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro yatakuwa kwenye mchakato wa kuwachagua wabunge wao baada ya waliokuwepo kujiuzulu.

Video: Kwenye vituo vya Uchaguzi Hali ikoje?

Vile vile, uchaguzi huo utafanyika kwa Madiwani katika Kata nane Tanzania Bara na kuhusisha wapiga kura 355,131 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kutakuwa na vituo vya kupigia kura 867.

 

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema leo asubuhi saa 2:00 huku wananchi wakijitokeza kuchagua viongozi wawakilishi wao na ulinzi ukiwa umeimarishwa na jeshi la polisi.

Katika Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia wa CCM anachuana na Salum Mwalimu wa Chadema ambapo Siha, Elvis Christopher Mosi wa Chadema akichuana na Dkt. Godwin Ole Mollel wa CCM.

 

 

Global TV Online itakuwa mubashara kukuletea matukio yote yatakayokuwa yanajiri kwenye uchaguzi huo, Kinondoni na Siha.

LIVE: MGOMBEA UBUNGE CCM ‘MAULID MTULIA’ AKIPIGA KURA YAKE – (VIDEO)

 

Comments are closed.