The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi wampa likizo JB

0

JB (2)Imelda Mtema

LIKIZO! Mkongwe wa sinema Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa amelazimika kujipa likizo ya lazima kwa kutofanya shughuli za sanaa hadi pale uchaguzi utakapopita.

JB (1)Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, JB alisema ameamua kusimama kazi zake za sanaa kwani kwa sasa kila mtu anawaza mambo ya uchaguzi na hakuna chochote anachoweza kufanya kikapokelewa bila ushabiki wa vyama.

“Nimeweka kila kitu pembeni mpaka uchaguzi huu umalizike maana kila mtu yuko bize na mambo ya uchaguzi, huyu anasema hivi huyu anasema vile, tumuombe tu Mungu atuvushe salama na mambo yetu yaendelee kama kawaida,” alisema JB.

Leave A Reply