The House of Favourite Newspapers

Uchebe: Nimempa Shilole Talaka Tatu, Akae Eda

0

FUNDI gereji na mfanyabiashara Uchebe amefunguka kinachondelea baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa mkewe, msanii Shilole, ambapo amesema ametoa talaka za awamu hivyo anamtaka Shilole akae eda ili kupatiwa huduma.

 

Akizungumza na East Africa Radio, Uchebe amesema hawezi kusema kama ndoa ni mbaya kisa imeingia dosari kwa sababu ndoa ni jambo la kheri japo  vijana wanakutana na mambo mengi.

 

“Matatizo yanaponikuta huwa namuomba sana Mungu nisifanye jambo la ajabu, maana wanawake wana vitu viwili; kwanza anapomkosea mumewe hakubali anataka kushindana naye na kwenye ndoa ndiyo inawabeba sana,” amesema Uchebe.

 

Aidha, ameendelea kusema: “Mitihani ipo na inatokea, ni moja ya hatua kwenye maisha, sasa hivi nimejipunguza kidogo sipo karibu na mwenzangu na nimetoa talaka ambazo zina awamu pia anatakiwa akae eda ili kupata huduma, ukitaka kuoa kuna misingi mingi unatakiwa kuifuata.”

 

Leave A Reply