The House of Favourite Newspapers

Uchumba wa Ariana Grande na Pete Davidson Wayeyuka!

Image result for ARIANA GRANDE & PETE DAVIDSON

UCHUMBA wa kuvishana pete kati ya mwimbaji na mwigizaji wa kike wa Marekani, Ariana Grande (AG) na mwigzaji/mchekeshaji,  Pete Davidson (PD),  umeyeyuka na haupo tena.

Vyanzo vya uhakika kati ya AG na PD vimesema mipango hiyo ya ndoa imevunjika, wawili hao wakisema hawakuwa tayari kwa uhusiano huo japokuwa wataendelea kupendana tu.

Wawili hao walitangaza sapraiz ya kuchumbiana mwezi Mei mwaka huu ambapo Grande alivishwa pete yenye thamani ya Dola 100,000 (Sh. mil. 228) lakini alibadili nia baadaye.

Related image

Mara ya mwisho wawili hao walionekana wakiwa pamoja wiki iliyopita.  Hata hivyo, kuna uvumi kwamba uwezekano wa kuoana bado upo kwa kiasi fulani.

Comments are closed.