Uchumba wa Ben Pol watikiswa!

DAR ES SALAAM: “Mitandao ya kijamii imejaa watu wanaotamani kumuona mtu anaharibikiwa kisha wanasherehekea!” Hayo ni maneno ya mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’, Anerlisa Muigai akionesha kutikiswa kwa uchumba wao.

 

Kwa mujibu wa mrembo huyo, ndilo somo ambalo amejifunza ndani ya kipindi cha muda mfupi alichodumu kwenye uchumba na Ben Pol.

 

Anerlisa anasema amegundua hilo baada ya kukaa kwa siku tano bila kuposti chochote kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram ambapo watu walianza kufikiri kuna tatizo huku wakieneza kuwa uchumba wake na Ben Pol umevunjika.

 

“Inachekesha, nimekaa siku tano bila kuposti chochote na watu tayari wameanza kuamini kuna tatizo na wengine kunitumia mistari ya kwenye Biblia.

“Nimegundua watu wengi wanasubiria anguko la mtu ili washerehekee,” alisema Anerlisa.

 

Anerlisa aliongeza kwamba, amejifunza kuwa kuna mashetani wengi na wenye wivu waliojaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zaidi alisema kama mtu akisikiliza sana maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii anaweza kujikuta kwenye wakati mgumu kiasi cha kuchanganyikiwa.

 

“Mitandao ya kijamii ni sehemu ambayo mtu unapaswa kujisimamia mwenyewe. Nitakuwa ninajaribu kuposti kazi zangu za kila siku za kawaida ambazo watu wanatarajia. Halafu matukio mengine labda nikiwa mahali fulani na watu ninaowapenda na kuwajali kwa sababu kuna watu wengi wanaowaza mabaya na wenye wivu kwenye mitandao ya kijamii, lazima nijisimamie la sivyo nitakuwa kichaa kama nikisikiliza kila kinachosemwa kutegemeana na maisha ya watu kwenye mitandao ya kijamii.

 

“Watu wengi wanaonesha asilimia 15 tu ya maisha yao halisi kwenye mitandao,” alisema Anerlisa.

Anerlisa wa Kenya ambaye ana utajiri mkubwa na Ben walikutana mwaka jana kisha kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kabla ya kuchumbiana na sasa inasubiriwa shughuli kubwa ya ndoa.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Loading...

Toa comment