The House of Favourite Newspapers

UCHUMBA WA TUNDA, CASTO CHALI

LICHA ya hivi karibuni kujinadi kwamba anampenda mchumba wake na wana malengo kibao, lile penzi la mtangazaji wa Runinga ya Clouds, Casto Dickson na video queen maarufu Bongo, Tunda Sebastian limepiga mwereka chali.  Chanzo makini kililieleza Risasi Mchanganyiko kuwa, penzi la wawili hao ambalo lilikuwa ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na jinsi walivyokuwa wakijiachia viwanja tofauti, lilivunjika hivi karibuni huku sababu zikiwa hazijulikani.

Chanzo hicho kilitonya kuwa, kutokana na kuvunjika huko ndiyo maana hata siku hizi hawaaniki picha wakiwa pamoja viwanja kama zamani ambapo wamekuwa wakifanya siri, hawataki watu wajue kama wameachana. “Unajua lile penzi la Tunda ambaye anajiita boss baby na Casto limevunjika na kila mmoja sasa hivi ana maisha yake ndiyo maana huwaoni tena pamoja, ninyi fuatilieni mtapata ukweli,” kilisema chanzo.

Related image

TUNDA AFUNGUKA

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Tunda kwa njia ya simu na kumsomea madai ya uchumba wake na Casto kuvunjika ambapo alifunguka kuwa, kwa sasa yupo singo yaani hana mpenzi.

Alipoulizwa sababu za kutokuwa na mpenzi wala mchumba ni nini wakati Casto hivi karibuni alimmwagia sifa kibao kwenye runinga akisema kwamba wana ndoto kubwa za maisha, mwanadada huyo alisisitiza kwamba hana mpenzi wala mchumba. “Jamani ni hivi, kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, nipo bize sana, nina vitu vingi zaidi ya uhusiano,” alisema Tunda.Image result for casto dickson na tunda

CASTO APATA KIGUGUMIZI

Ili kuujua ukweli wa kauli ya Tunda na habari hizo za madai ya uchumba wao kuvunjika, gazeti hili pia lilimtafuta Casto na kumuuliza ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Haaa…nani kakuambia… Tunda ndiyo amekiri hivyo? Hebu ngoja kidogo….akakata simu! Baada ya muda akapigiwa tena na kupokea: “Kama mapenzi yetu yamevunjika watu wataona tu ila kwa sasa tumeamua vitu vyetu viwe siri ‘private’ sana, achaneni na hii kapo kabisa.”

Tunda na Casto wamekuwa na mapenzi motomoto huku wakijianika mitandaoni kimahaba, lakini kwa sasa hawafanyi hivyo.

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko

 

Comments are closed.