The House of Favourite Newspapers

Uchumba wa wema, Mnamibia chali!

0

cvWema Sepetu ‘Madam’ akiwa na mpenzi wake  Mnamibia Luis Munana.

Brighton Masalu na Imelda Mtema
KISICHO riziki hakiliki. Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia lile penzi lililochipua kwa kasi na kutikisa Jiji la Dar kati ya Wema Sepetu ‘Madam’ na Mnamibia Luis Munana kudaiwa kuvunjika huku ‘bibie’ akidaiwa kuhamishia ‘majeshi’ kwa bwa’ mdogo mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshot 2014, Idris Sultan, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.

Kama njiwa apelekaye ujumbe wa mahaba akitumwa, ndivyo mmoja wa mashosti wa karibu sana na Wema kwa siku hizi, alivyomwaga ‘ubuyu’ wa kuwepo kwa hali hiyo ya sintofahamu juu ya wawili hao.

a

Wakipozi kimahaba.

Mwandishi wetu akiwa ofisini akiwajibika kama kawaida, ghafla simu ya mezani iliita na alipoipokea, mambo yalikuwa hivi;
Mtoa taarifa: Eeh, nyie Risasi Mchanganyiko mpo?
Risasi Mchanganyiko: Tumejaa tele, tukusaidie nini?
Mtoa taarifa: Hivi mna habari?

Risasi Mchanganyiko: Zimejaa tele ila hata hiyo yako tunaihitaji, leta maneno.
Mtoa taarifa: Kwa taarifa yenu lile penzi la Wema na yule Mnamibia limefika mwisho, kwa sasa Wema amehamishia mahaba niue kwa Idris.

Risasi Mchanganyiko: Huyuhuyu wa Big Brother?
Mtoa taarifa: Kama ulivyomalizia, Mnamibia wa watu analia tu, ila tafadhali sana usinitaje mahali popote (akakata simu).

WEMA17Baada ya ‘kubugia ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi, aliposomewa madai hayo, haraka sana kwa sauti ya kupayuka alisema;
“Jamani, sitaki kuzungumzia upuuzi huo, tafadhalini sana mtu asifuatefuate maisha yangu, sitaki na ningejua unataka kuniuliza upuuzi kama huo, I swear (naapa), nisigepokea kabisa simu yako (akilitaja jina la mmoja wa waandishi wetu).

Ili kujiridhisha kwa kina zaidi, gazeti hili liliamua kumtafuta Idris ili naye aseme chochote, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa, jitihada za kumsaka zinaendelea, akiingia kwenye ‘rada’ zetu, data zitawekwa hadharani.

Wema na Munana walianzisha urafiki wa kimahaba mara baada ya jamaa huyo kushiriki Shindano la Big Brother ambapo mahaba yao yalichomoka hadharani kwa mara ya kwanza Juni mwaka huu katika Viwanja vya Posta jijini Dar kulipokuwa na sherehe ya Instagram.

Leave A Reply