UDART Yatoa Mwongozo wa Kujikinga na Corona kwa Abiria Wake

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa Mwongozo kwa Watumiaji wa Magari ya Mwendokasi ili kujikinga na maambukizi ya #CoronaVirus.

Wasafiri wanaotumia Magari ya Mwendokasi wanatakiwa kuvaa barakoa hususani asubuhi na jioni na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu wakati wa kusubiri usafiri.

 

Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi vinawekewa maji na sabuni ambayo kila msafiri atatakiwa kunawa mikono. Pia, watu wametakiwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

 

Aidha, wasafiri wanatakiwa kusubiri basi lingine ikiwa basi lililofika limejaa

Toa comment