The House of Favourite Newspapers

UEFA: Man United, Man City zachapwa

0

2C5AE92C00000578-3235796-image-a-41_1442349707282Wachezaji wa  Juventus wakishangilia baada ya kushinda bao la pili dakika ya 81.

2C5A83B100000578-3235796-image-a-12_1442347426680

Kiungo wa Juventus, Pogba (kushoto) akimtoka Samir Nasri.

2C5A6E6B00000578-0-image-a-9_1442346801906

Mshambuliaji wa Man City,  Wilfried Bony akiwa chini baada ya kupata maumivu ya goti.

Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la klabu bigwa barani Ulaya baada ya kuchapwa.

Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Psv.Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akifunga bao la ushindi.

Man City nao wakiwa katika Dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee ya Turin Juventus mabao ya Juve yakifungwa na Álvaro Morata na Mario Mandzukic huku bao la kujifunga la beki Giorgio Chiellini,likiwapa Man City bao moja.

Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa kishindo kwa ushindi wamabao 4-0 dhidi ya Shakt Donetsk, Cristiano Ronaldo akifunga hattrick na Karim Benzema akifunga bao moja.

Matokeo mengine ya michuano hii ni:

Psg 2 – 0 Malmö FF

VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA

Benfica 2 – 0 FC Astana

Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid

Sevilla 3 – 0 Borussia Mönchengladb

Leave A Reply