The House of Favourite Newspapers

Ufafanuzi Kuhusu Uhamisho Wa Mpiana Monzinzi

0

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuhusu suala la mchezaji wao mpya Mpiana Monzinzi, kutoka FC Lupopo ya DRC ambapo imekuwa ikielezwa kuwa kuna matatizo ya kwenye makubaliano ya kupata saini yake na timu yake ya zamani.

Kuna taarifa ambayo imekuwa ikisambaa na inaonekana imetolewa na FC Lupopo, inamlalamikia Monzinzi kuondoka bila ruhusa na kusaini mkataba na klabu ya Azam FC bila wao (FC Lupopo) kuwa na taarifa.

 

Azam FC imewekwa ukweli namna hii ili kuwaomnoda hofu mashabiki wake:-

“Kimsingi sisi Azam FC, tumemnunua mchezaji huyu kutoka Klabu ya Academic Club Rangers, ambayo ndiyo inayommiliki.

“Huko Lupopo alienda kwa mkopo ambao ulitakiwa kukamilika Juni mwaka huu.Lakini ACR ambao ndiyo wamiliki halali, wametuuzia mchezaji huyo kwa vielelezo vyote.

“Ni jukumu la ACR na Lupopo kuwasiliana na kuliweka sawa swala hili.Tumewasiliana na ACR kupitia Rais wao, Lambert Osango Nsenga, ambaye kimsingi ndiyo mmiliki halisi wa mchezaji huyu.

 

“Asilimia kubwa ya wachezaji wa DRC humilikiwa na watu, na hao watu huwapeleka wachezaji hawa kwenye vilabu mbalimbali kwa mkopo ili kutengeneza soko.

“Bwana Lambert amesema hawajawapelekea Lupopo taarifa rasmi, lakini tusiwe na wasiwasi, watafanya hivyo baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

“Tunawaomba mashabiki wetu mfurahie kwa amani sikukuu ya Krisimasi na Mwaka mpya, mkiwa na uhakika kwamba Mpiana Monzinzi ni mchezaji wetu halali.

“Tunawaomba mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi, kila kitu kilo kwenye udhibiti,” ilieleza taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC.

Leave A Reply