UFAFANUZI: Televisheni za Mtandaoni Tu Ndio Zifunguliwe

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Aprili 7, 2021 ametoa ufafanuzi wa vyombo vya habari vinavyotakiwa kufunguliwa kutokana na maelekezo ya Rais Samia.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria” amesema Msigwa.

 

 

Toa comment