The House of Favourite Newspapers

Ufafanuzi wa TCRA Kuhusu Maudhui ya Vyombo vya Nje

0

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitaka vyombo vya habari vya ndani ya nchi vyenye leseni ya kurusha matangazo kuhakikisha vina kibali cha kurusha matangazo ya vituo vya kimataifa kutoka katika mamlaka hiyo kabla ya kufanya hivyo.

 

TCRA imesema hayo wakati ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni mpya ambazo miongoni mwa mambo mengi zinazuia chombo cha habari cha ndani ya nchi kurusha matangazo ya chombo cha habari cha nje bila kuwa na kibali.

 

Mamlaka hiyo imesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kusimamia maudhui ya nje yanayorushwa mbashara nchini Tanzania na kwamba huo ni utaratibu wa kawaida wenye lengo la kuleta ufanisi katika usimamizi wa matangazo.

 

Kanuni hiyo imekuja wakati vyombo mbalimbali vya Tanzania vimekuwa vikirusha matangazo ya vyombo vya kimataifa kama vile BBC Swahili, Sauti ya Amerika na Deutsche Welle.

 

Hivi karibuni Radio Free Africa ilipewa wito wa kufika mbele ya TCRA kujieleza kwanini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka kanuni za utangazaji kufuatia matangazo iliyorusha wakati wa kipindi cha BBC Swahili.

Leave A Reply