The House of Favourite Newspapers

Uganda: Msichana Miaka 11 Abadili Maumbile Kuwa Mvulana

BINTI wa miaka 11, aliyefahamika kwa jina la Catherine amefanyiwa upasuaji na kubadili maumbile yak ya uzazi kutoka usichana kuwa mvulana.

 

Imeelezwa kuwa, upasuaji huo wa Kihistoria nchini Uganda umefanyika kwa mafanikio makubwa katika Hospitali ya Mulago chini ya Kliniki ya Endocrinology.

 

Catherine alizaliwa akiwa na jinsi ya Kike na kulelewa kama mtoto wa kike, lakini kadiri siku zinavyokwenda sehemu ya uke wake ilianza kubadilika na kuota uume.

 

Kwa mujibu wa uchunguzi wa wataalamu wameeleza kuwa mabadiliko hayo yamesababishwa na uwepo wa homoni nyingi za kiume kuliko za kike. Msichana huyo alipewa jina la Catherine lakini baada ya upasuaji huo amebadili jina na kuitwa Emma.

Comments are closed.