The House of Favourite Newspapers

Ugonjwa wa endometriosis unaowasumbua wanawake-2

0

Blausen_0349_EndometriosisWIKI iliyopita tuliangalia utangulizi wa tatizo hilo la Endometriosis, kwanza niliwaeleza kuwa tatizo hili linawasumbua wanawake na hutokana na pale ambapo seli na tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa uzazi (endometrium), zinajijenga na kukua nje ya tumbo la uzazi.

Seli na tishu hukua na kujificha katika eneo la nyonga (pelvis), tumbo la chini (abnomen) na kwenye ovari na ni mara chache ugonjwa kusambaa kwenye viungo vingine zaidi ya nyonga fuatilia makala haya utapata maarifa muhimu juu ya tatizo hili la Endometriosis.

Dalili za ugonjwa wa Endometriosis
Maumivu- Hii ndiyo dalili iliyo kuu kwa wanawake wenye ugonjwa huu. Mwanamke asiye na tatizo hili huweza pia kupata maumivu wakati wa kuona siku zake za hedhi lakini maumivu hayo huwa siyo makali kama ya mwanamke aliye na ugonjwa huu. Maumivu haya yanaweza kuwa ya aina tofauti:-

¬Maumivu makali ya hedhi: Maumivu haya huongezeka kadiri muda unavyokwenda.
¬Maumivu wakati wa tendo la ndoa, ambayo ni makali na ni tofauti na maumivu ambayo mwanamke anaweza kupata pale anapoingiliwa na mwanaume anapoanza kufanya tendo la ndoa.

¬Maumivu ya muda mrefu ya chini ya mgongo pamoja na nyonga.
¬Maumivu ya tumbo.

¬ Maumivu wakati wa kupata haja kubwa au haja ndogo, na hii hutokea wakati wa hedhi. Na pia ni mara chache sana mgonjwa anaweza kuona damu katika haja kubwa au ndogo.

Kuona damu ya hedhi katikati ya mzunguko- Endapo hali hii itajitokeza mara kwa mara ni vizuri kumuona daktari wako kwa ushauri zaidi.
Matatizo ya mmeng’enyo- Matatizo haya huambatana na kuhara, kukosa choo, tumbo kujaa, kichefuchefu na haya yote mara nyingi hutokea wakati mwanamke anapoona siku zake za hedhi.

Haiwezekani kuzuia ugonjwa huu wa Endometriosis. Lakini unaweza kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huu kwa kupunguza kiwango cha homoni ya Ostrogeni mwilini. Homoni ya Ostrogeni husaidia kujenga na kunenepesha ukuta wa kizazi wakati wa mzunguko wa hedhi.

Jinsi gani ya kupunguza kiwango cha Ostrogeni mwilini?
¬Ongea na mfamasia wako kujua ni dawa gani za uzazi wa mpango kama vidonge, vibandiko au vipandikizi vyenye kiwango kidogo cha homoni ya Ostrogeni.
¬Fanya mazoezi kila siku, hii itasaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini. Mazoezi ya mara kwa mara hupunguza mafuta na hii husaidia kupunguza kiwango cha Ostrogeni mwilini.

¬Epuka vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha kafeini, tafiti zinaonesha kuwa unywaji wa vinywaji hivi kama kahawa, soda na vingine vyenye kafeini kwa kiwango kikubwa huongeza kiasi cha homoni ya Ostrogeni mwilini.

¬Epuka unywaji wa pombe kupindukia, pombe huongeza kiasi cha Ostrogeni mwilini, kwa wanawake wanaochagua kunywa isiwe zaidi ya kinywaji kimoja kwa siku.
Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vyema ukafuatilia makala haya. Nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume. wKwa maelezo na msaada usisite kupiga simu au kuwatembelea katika vituo vyao.

Leave A Reply