Ugonjwa wa kipindupindu

070615_cholera_THUMB_LARGELeo tutachambua ugonjwa wa kipindupindu unaozikumba jamii mbalimbali na kuathiri nchi nyingi za Kiafrika Tanzania ikiwemo.

Ugonjwa wa kipindupindu ni tatizo kubwa la kiafya kwa nchi zinazoendelea, ambako milipuko yake hutokea kufuatana na misimu ya hali ya hewa na kuhusishwa na suala la umaskini na usafi duni.

gonjwa huo husababisha mtu kuharisha choo kingi cha maji maji ambacho hufanya maji kupungua haraka mwilini hali ambayo kitaalam huitwa Dehyadration.

Iwapo mtu huyo aliyeambukizwa kipindupindu hatapata matibabu ya haraka, huweza kupoteza maisha.

Wataalam wa afya wanasema kuwa asili ya kipindupindu ilianzia nchini India mwaka 1826, ambapo kufikia mwaka 1830, kila mwaka watu elfu 40 walikuwa wakifariki dunia kwa maradhi hayo.

Ugonjwa wa kipindupindu ulifika Afrika mwaka 1970 na kuenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ya bara hilo.

Ilipofika mwishoni mwa mwaka 1971, nchi 25 za Kiafrika ziliripoti kukumbwa na milipuko ya kipindupindu.

Sasa tuangalie vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kipindupindu. Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio Cholerae ambacho kina sumu mbili maalum.

Sumu moja imeelezwa kuwa inasababisha kuhara kusikosita na nyingine huvisaidia vimelea vya ugonjwa huo kuishi na kuendelea kuzaliana katika utumbo wa mwanadamu.

Vimelea hao huweza kuishi ndani ya matumbo ya watu walioambukizwa kwa muda wa siku 7 hadi 14, bila ya watu hao kuonesha dalili kali au kutoumwa kabisa. Kipindupindu ni ugonjwa unaomsababishia mtu hali ya kuendesha sana.

Ugonjwa huu pia huenezwa kwa kasi na maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha mwanadamu.
Itaendelea wiki ijayo kwenye gazeti hili hili.

Loading...

Toa comment