The House of Favourite Newspapers

Ugonjwa wa Usonji Kwa Watoto (Autism)

USONJI au Autism kwa kitaalamu, ni tatizo linalowasumbua watoto wengi lakini kwa bahati mbaya, jamii hvaina uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huu, dalili zake na matibabu hivyo kusababisha mateso makubwa kwa waathirika wa ugonjwa huu.

Usonji, ni ugonjwa unaoanza kuonesha dalili zake kwa mtoto anapofi kisha umri wa kuanzia miaka mitatu ambapo mtoto huwa mzito kuelewa mambo kama watoto wengine, hapendi kuchangamana na wenzake, hawezi kujieleza kwa maneno anachokitaka na badala yake, anatumia zaidi ishara au lugha ya picha.

Mtoto mwenye usonji, huwa mzito kuzungumza, au akianza kuzungumza huwa na kawaida ya kurudiarudia neno moja kwa muda mrefu, au kurudia walichokisema watu wengine na huwa na tabia tofauti kabisa na watoto wengine.

Hupenda kucheza mchezo mmoja kila siku, tena peke yake na kama nilivyosema, huwa mgumu kuelewa jambo lakini akilielewa, hulielewa kwa ufasaha na kwa undani kuliko watu wengine  wote.

Watoto wa namna hii, huwa na uwezo mkubwa darasani kama wakiendelezwa vizuri na hata wakiamua kubobea kwenye jambo fulani, huwa na ujuzi mkubwa kuliko mtu mwingine yeyote.

Ili kumgundua mtoto mwenye tatizo hili, wazazi wanatakiwa kuwa karibu na kufuatilia tabia na mwenendo wa watoto wao.

Wataalamu wa afya duniani hawajaweza kubaini chanzo cha ugonjwa huo kwa watoto lakini tatizo hilo huanza kuonekana kwa mtoto pale anapofi kisha umri wa miaka mitatu ambao ndio umri mtoto anatakiwa kuanza kuonyesha uwezo wake wa kutambua vitu, kuiga tabia na kujifunza vitu mbalimbali.

Dalili nyingine za ugonjwa huo ni mtoto kushindwa kuwatazama watu machoni, kuwa na tabia ya utukutu, kupenda kukaa peke yake na kupata ugumu wa kutumia viungo vya mwili, kwa mfano kuendesha baiskeli, kupanda ngazijapo hawana ulemavu wa viungo.

Mpaka sasa haijafahamika kama watoto wanazaliwa na usonji au hupata madhara baada ya chanjo. Mtoto mweye usonji huwa mara nyingi akili yake inakuwa ‘slow’ kulinganisha na watoto wengine wa umri wake wasio na usonji.

Pia usonji huathiri jinsi akili inavyotuma na kupokea ujumbe kwenye milango ya fahamu ndiyo maana watoto wengine wenye usonji hawawezi kutafuna chakula, hawapendi nguo za aina fulani, hawapendi kuguswa au hawapendi kelele.

Itaendelea wiki ijayo!

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.