The House of Favourite Newspapers

Uhakiki Laini za Simu Mwisho Februari 13, 2023 Waziri Nape Afunguka – Video

0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

SERIKALI imeongeza siku 14 kwa Watanzania waliosajili laini zao za simu kuhakiki laini hizo kabla ya kufikia tarehe 13 Februari, 2023 saa 10 jioni ambapo laini zote ambazo hazijahakikiwa zitazimwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka wimbi la matapeli wanaotumia laini zilizosajiliwa kutapeli watu na wengine kufanya matukio ya kihalifu.

Akizungumza na waandishi Januari 24, 2023 jijini Dodoma Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema sekta ya mawasiliano inakua na mpaka zipo laini za simu zinatotumika zaidi ya milioni 60.

Amesema hadi kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi kufikia tareh 19 Januari, 2023 laini milioni mbili zilikuwa hazijahakikiwa.

“Serikali kupitia TCRA tulichukua hatua za kufanya usajili wa laini za simu kwa kutumia biometric – alama za vidole na vitambulisho vingine ambapo dirisha lilifungwa tarehe Mei, 2019 na lilifungwa Disemba 2021.

“Tulianzisha kampeni ya kuhakiki laini hizo na hadi sasa zoezi linaendelea kwani mwanzoni ilikuwa tuende hadi mahali lakini tukaongeza muda mara mbili na ya tatu ambayo ilikuwa ya mwisho ni tarehe 31 Januari, 2023.
Amesema kwa kuwa kuna laini nyingi mtaani ambazo watu wametumia vitambulishi vya watu wengine kusajili, sasa zitaenda kuzimwa hivyo wanatakiwa kuhakiki laini hizo ili kutokomeza utapeli wa ‘ile pesa tuma kwa namna hii’ .

“Tunaenda kuzima ambazo zimesajiliwa lakini zimesajili kwa uongo, kama huzijasajiliwa kwa uongo nenda kaihakiki laini yako, yeyote aliyesajili kwa uongo hawezi kuihakiki kwa sababu mfumo utamuumbua, hivyo tumeongeza siku 14.

“Mpaka tarehe 13 Februari siku moja kabla ya siku ya wapendanao tunataka anga la mawasiliano liwe salama, iwe siku ya furaha.. watu wakae wakiwa salama,” amesema Nape.

Leave A Reply