Ripoti ya kamati ya bunge nchini Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.
Kamati hiyo ya Mambo ya Nje imesema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zingewakumba raia baada ya serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na maasi.
Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumiwa kama fursa ya kubadilisha utawala, ripoti hiyo inasema.
enzi za uhai wake, Muammar Gaddafi
Ripoti hiyo inamtuhumu aliyekuwa waziri mkuu wakati huo David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahsusi kuhusu Libya baada ya kuuangusha utawala wa Gaddafi.
Wabunge hao wanasema hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mzozo wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika kaskazini
Msemaji wa serikali ya Uingereza ameitetea serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, pamoja na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.
Gaddafi aliuawa na waasi 20 Oktoba, 2011 kwenye mji aliozaliwa wa Sirte nchni Libya.
Comments are closed.