Uingereza Yashutumu Harakati za Urusi Katika Kiwanda cha Kuzalisha Nyuklia cha Zaporizhzhia

Kiwanda cha Zaporizhzhia

UINGEREZA imesema kuwa, hatua zilizochukuliwa na Urusi kwenye kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia huenda zikahatarisha na kudhoofisha usalama wa kiwanda hicho.

 

Pia Uingereza imesema kuwa, nia ya Urusi kuhusu kiwanda hicho bado haijulikani wazi baada ya miezi mitano ya Urusi kuinyakua Ukraine, Vikosi vyake vinafanya kazi kwa ukaribu na Mikoa iliyo karibu na Kiwanda hicho cha Kuzalisha nguvu ya Nyuklia.

Kiwanda cha Zaporizhzhia kinachotengeneza Nyuklia nchini Ukraine

Uingereza ilisema katika chapisho la Kijasusi kwenye Ukurasa wa Twitter kwamba:

 

“Vikosi vya Urusi labda vimetumia eneo kubwa la Kituo, haswa katika Jiji la Adja Cent la Enerthodar kupumzisha vikosi vyao kwa kutumia ulinzi wa nguvu ili kupunguza hatari kwa vifaa vyao na Wafanyakazi kutokana na mashambulio makali ya yanayofanywa na Ukraine wakati wa Usiku.”

Urusi imetumiakiwanda hicho kuvipatia nguvu vikosi vyake vya mizinga kutekeleza mashambulizi

Aidha Uingereza imesema kuwa Urusi inatumia eneo hilo ili kuviwezesha vikosi vyake vya Mizinga vilivyoko katika maeneo hayo kuyalenga na kuyapiga maeneo ya Ukraine yaliyo karibu na ukingo wa Magharibi upande wa Mto Dnipro.

 

 3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment