The House of Favourite Newspapers

Msikiti wa Samatta Waanza Kutumika – Video

0

WAKAZI wa Vikindu Kidubwa Mkoa wa Pwani, wameanza kuutumia msikiti unaojengwa na mshambuliaji wa Fenerbahce, Mtanzania, Mbwana Samatta, licha ya kutokamilika.

 

Samatta alianza kuujenga msikiti huo mwaka 2018 wakati akiitumikia KRC Genk ya Ubelgiji aliyojiunga nayo akitokea TP Mazembe, kabla ya kwenda Aston Villa na sasa akiwa Fenerbahce.

Spoti Xtra limefanikiwa kuutembelea msikiti huo na kuona maandeleo ya ujenzi wake ambapo mafundi wanaendelea na kazi, huku watu wakianza kuutumia katika ibada za kila siku.

Mmoja wa mafundi waliokuwa wakiendelea na ujenzi katika msikiti huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Shaaban, alisema: “Ujenzi unaendelea, umefi kia katika umaliziaji ikiwemo kuweka milango na kupaka rangi.

 

“Kubwa zaidi ni kwamba wakazi wa hapa wameanza kufanya ibada za kila siku isipokuwa Swala ya Ijumaa pekee kwa kuwa bado haujaisha kabisa, ukiisha swala zote zitakuwa zikiswaliwa.”

STORI: IBRAHIM MUSSA NA JULIUS RICHARD, Dar es Salaam

 

Leave A Reply