The House of Favourite Newspapers

Ujue ugonjwa mpya wa kisonono

0

princ_rm_photo_of_genital_warts

Wasomaji wa safu hii, wiki hii tunawaletea taarifa nzito kuhusu usugu wa dawa kwa wenye ugonjwa wa kisonono.

Taarifa ya tahadhari iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni imesema, kumegundulika aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono maarufu kama “gono” ambavyo vinahimili nguvu za dawa (Resistant to Drugs) zinazotumika kutibu ugojwa huo.

Tahadhari hiyo ya WHO imesema ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa siku zijazo.

Dalili
Dalili ni mgonjwa kutokwa na usaha sehemu za siri (kwa wanaume) na kwa wanawake kusikia maumivu ya chini ya tumbo. Kutokwa na vidonda kwenye ulimi au midomoni, macho kuwa na rangi nyekundu nakadhalika.

Shirika hilo la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatiliaji wa aina hiyo ya kisonono kutokana na ugonjwa huo kuwa na athari nyingi kwa binadamu kama vile mgonjwa kushindwa kupata mtoto (ugumba), mcharuko (Inflammation), wajawazito kujifungua watoto wenye ugonjwa wa macho na huweza kusababisha vifo.

Aina hiyo mpya ya vimelea vya kisonono vinaonesha usugu dhidi ya dawa zote za antibayotiki zinazotumika kutibu maradhi hayo ikiwemo dawa za jamii ya (Cephalosporins) ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa huo.
Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply