The House of Favourite Newspapers

Ujue ugonjwa mpya wa kisonono – 2

0

gonorrhea-2WIKI iliyopita tuliishia katika kuzungumzia dalili ya ugonjwa wa kisonono (gono), leo tunaendelea na sehemu yetu ya pili na ya mwisho, msomaji wetu fuatilia sehemu hii ili upate elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu unaoweza kukuletea matatizo katika afya yako.

Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidi ya dawa aina ya (Cephalosporins) viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hong Kong na Norway.

Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibayotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea mazingira mapya ndiyo chanzo kikuu cha kutokea kwa usugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono kusambaa kwa sasa duniani bila kuweza kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu  mzuri wa wagonjwa wake.

Elimu ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya kondomu inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono.

Leave A Reply