The House of Favourite Newspapers

Ujumbe Mzito wa Makonda Kuhusu Mtoto Wake – VIDEO

IKIWA ni takribani saa 24 tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mkewe wafanikiwe kupata mtoto wa kiume, kiongozi huyo amefunguka na kuandika ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu mtoto wake huyo aliyempa jina la Keagan.

 

Mara nyingine unapopewa mtihani haupimwi wewe ila wale wanaokuzunguka, kupitia mtihani wako watatokea watabiri, wazungumzaji na watu wa kila aina hadi watakaojivisha U-Mungu kiasi cha kufikia kukufukuru mara nyingine, lakini yote ni MUNGU anawapima imani ili aweze kuonesha UKUU WAKE, na anawakusanya kwa wingi ili atakapotenda NENO LAKE lisambae, hivyo sio kila mtihani ni wa kwako.

Na naomba nikiri Kupitia Keagan nimeuona UKUU WA MUNGU, tena MUNGU yule yule asieacha neno lake likaanguka, na kwa unyenyekevu mkubwa kwa hii furaha yote aliyoniletea narudisha sifa na utukufu kwake yeye alie juu.

Lakini pia kwa moyo mkunjufu kabisa nitoe shukran kwa kila mmoja aliejitoa kufurahi na kushukuru pamoja nami kupitia message, simu, post na hata maombi ya chini, tunasema asante sana sana na kupitia nyinyi nimeshuhudia Baraka nyingine ya WATU, kikubwa mtambue nathamini sana sana na kwa niaba ya mke wangu na familia kwa ujumla tunawashuru kutoka moyoni na MUNGU AWABARIKI SANA.

#BabaKeagan

Comments are closed.