The House of Favourite Newspapers

Diamond Amtumia Ujumbe, Zawadi ya ‘Wapendanao’ Mpenzi Wake

 

MSANII Naseeb Abdul Juma maarufu kama Diamond Platnumz ameisherehekea na kuimaliza Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) vizuri  kwa kutuma zawadi na kuandika ujumbe wa mahaba kwa mpenzi wake Tanasha Don.

 

Diamond ameweka picha katika akaunti yake ya Instagram iliyoambatana na ujumbe unaosomeka, “Kwasababu wewe ni mpendwa wangu milele….natumaini utapenda zawadi yangu ndogo ya kushangaza…japo upo mbali lakini moyo wangu upo nawe kwaajili yako”.

Kwa upande wa mpenzi wake huyo toka Kenya Tanasha Don pia alishukuru zawadi aliyotumiwa na mpenzi wake huyo ambayo ilikuwa kwenye picha yenye maneno, ‘I love You Tanasha’ huku yakiwemo maua na box za zawadi.

 

 

“Asante mpenzi wangu, mimi ni mwanamke wa bahati sana kuwa na wewe katika hii dunia.  Maneno hayawezi kuonyesha jinsi gani ninavyojisikia kwa wakati huu”.   Aliandika Tanasha kwenye akaunti yake ya Instagram.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.