The House of Favourite Newspapers

Ukame Waua Waturkana, Mifugo Yafa kwa Njaa!

UKAME unaozidi kushika kasi katika maeneo mbalimbali yanayokaliwa na watu wa kabila la Waturkana nchini Kenya umesababisha kupoteza maisha ya watu na mifugo kila siku.

Katika kijiji cha Lojere Emoit, watu watano wamekufa kufuatia ukame wa muda mrefu ambao umeua idadi kubwa ya mifugo ambao ndicho tegemeo kubwa la kiuchumi la watu wa sehemu hiyo.

Balaa hilo limekikumba pia kijiji cha Nang’erelemunyan ambacho kinakaliwa pia na wafugaji wa kabila hilo.

“Tumepoteza wanaume watatu, mwanamke mmoja na mtoto kijijini Lojere Emoit.  Watu hao wamekufa kutokana na njaa na walizikwa kati ya Machi 11 na 13,” anasema Samuel Loperito mzee wa kijiji hicho alipozungumza na gazeti la The Standard.

Kuongezeka sana kwa joto hati kufikia nyuzijoto 38 kwa kipimo cha Celcius, kumelifanya eneo hilo kuwa katika mazingira mabaya ambapo mbuzi, ng’ombe na ngamia wamekuwa wakifa kutokana na kukosekana kwa malisho na maji.

 

LIVE | Kumekucha CHADEMA Wampongeza Rais MAGUFULI “Tunakuunga MKONO”

Comments are closed.