UKARIBU WA NANDY, BILLNAS WAZUA GUMZO!


S
IKU chache baada ya picha kusambaa zikiwaonesha wakali wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na William Lyimo ‘Billnas’, zimezua gumzo kwa mashabiki na kudhani huenda wamerudiana.

 

Katika picha ambayo Nandy aliiposti katika ukurasa wake wa Instagram, mashabiki walikuwa na hisia tofauti ambapo wengi wao walioneshwa kufurahishwa na kitendo cha wawili hao kuwa pamoja.

“Umeanza tena Nandy?”

“Mi’ naona uko na Nenga (Billnas) hapo, mh!” Zilisomeka baadhi ya meseji.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend kuhusiana na ishu hiyo, Nandy alisema hana kinyongo kabisa Billnas kwani walishamaliza tofauti zao tangu zamani hivyo kwa sasa wao ni washkaji tu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

 

“Mimi na Bill sasa hivi ni washkaji tu, hakuna chembechembe yoyote ya mapenzi kati yetu, tulishaachana muda mrefu na kila mtu ana maisha yake, sioni tatizo kuwa naye karibu,” alisema Nandy.

 

Wawili hao walishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi ambapo video yao wakiwa faragha ilivuja na Nandy kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

 

MEMORISE RICHARD | IJUMAA WIKIENDA

MWINGIRA: AMUOMBEA MAKONDA, AMWAGA MACHOZI

Toa comment