The House of Favourite Newspapers

Ukawa, CCM sasa lala salama

0

magufuli (5)VITA vya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu inazidi kukolea na kwa mujibu wa habari kutoka kambi mbili pinzani za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo vyama hivyo vinaanza ngwe ya lala salama.

Chanzo cha habari kilicho karibu na timu ya kampeni ya CCM, kimesema chama chao ndiyo kama kinaanza rasmi shughuli hiyo leo, kwani kinategemewa kuanza kutumia ‘silaha’ nzito ili kuhakikisha kinausambaratisha upinzani.

lowassaa“Jamaa wana helikopta zipatazo tano ambazo zimegawanywa kwa wana kamati kushambulia maeneo mengi kadiri wanavyoweza, lengo ni kuyafikia maeneo ya ndani na ambayo kidogo yanakuwa vigumu kupitika kwa njia ya barabara, katika siku hizi zilizobaki, kila eneo litafikiwa,” kilisema chanzo hicho.

Wakati kukiwa na taarifa hizo kutoka chama tawala, Ukawa nao wanasemekana kuandaa ‘majeshi’ yao ya maangamizi kwa kutumia jumla ya helikopta saba ambazo zitaanza kazi ya anga kwa anga ili kuwafikia wapiga kura katika hatua hii ya lala salama.

“Ni kweli, zimetayarishwa helikopta saba zitakazoanza zoezi kali la kutafuta kura katika hatua za lala salama, Hizi zimegawanywa kwa makamanda tofauti wa kuongoza mapambano, nina uhakika Lema (Godbless, Arusha) atakuwa nayo moja, Wenje (Ezekiel, Nyamagana), Msigwa (Mchungaji Peter, Iringa), Lissu (Tundu, Singida) kila mmoja atakuwa na chopa ya ‘kumwaga sumu’ kila kona ya Tanzania,” alisema kiongozi mmoja wa umoja huo, aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji.

 

Leave A Reply