The House of Favourite Newspapers

Ukawa Yashinda Umeya Kinondoni

0

1.Hali ilivyokuwa kwenye kikao hicho cha uchaguzi wa meye na naibu wake.Hali ilivyokuwa kwenye kikao hicho cha uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na naibu wake kilichofanyika katika Ofisi za Manispaa ya Kinondoni.
2.Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mnyika (katikati) akishiriki kikao hicho.Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (katikati) akishiriki kikao hicho.
4.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson (katikati) akiwa amehudhuria mkutano huo wa uchaguzi wa umeya wa Manispaa ya Kinondoni.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk.Tulia  Ackson (katikati) akiwa amehudhuria mkutano huo wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni.6.Zoezi la kupiga kura likiendelea.5.Wajumbe wa kikao hicho wakishiriki kupiga kura za kumtafuta Naibu Meya.Wajumbe wa kikao hicho wakishiriki kupiga kura za kumtafuta Naibu Meya.7.Zoezi la kuweka kura kwenye sanduku la kupigia kura likifanyika.Zoezi la kupiga kura likiendelea.8.Zoezi la kuweka kura kwenye sanduku la kupigia kura likifanyika.9.Wajumbe walioshiriki kupiga kura wa upande wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wakishangilia baada ya kumtangaza mshindi.Wajumbe walioshiriki kupiga kura wa upande wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakishangilia baada ya washindi kutangazwa.10.Kutoka kushoto ni Meya mteule wa Chama Cha Demokrosia na Maendeleo,Boniphace Jacob, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumnjuri, na Mwenyekiti wa usimamizi wa huo, Celestine Onditi.Kutoka kushoto ni Meya Mteule wa Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumnjuri na mwenyekiti wa usimamizi wa huo, Celestine Onditi.11.Meya mteule wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa cheti cha matokeo.Meya Mteule wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa cheti cha matokeo ya ushindi.12..Naibu meya mteule akizungumza jambo.Naibu Meya Mteule, Jumanne Amir akizungumza jambo.13.Wafuasi wa Ukawa walivyoonekana nje baada ya kumtangaza Meya wa manispaa ya kinondoni.Wafuasi wa Ukawa walivyoonekana nje baada ya kutangazwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni.14.Hali ilivyokuwa njeWafuasi wa Ukawa wakiwa nje ya Ofisi za Manispaa ya Kinondoni wakishangilia ushindi wa meya wao.15.Ulinzi ukiimalishwa eneo hilo.Ulinzi ukiimarishwa eneo hilo.

Hatimaye leo uchaguzi wa meya wa halmashauri wa Kinondoni  jijini Dar es Salaam umefanyika  ambapo diwani wa Ubungo kutoka UKAWA, Boniface Jacob (CHADEMA) amekuwa meya na na Naibu Meya  ni diwani wa Tandale, Jumanne Amir Mbunju (CUF).

Akitangaza matokeo Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Celestine Onditi alimtangaza mshindi wa Umeya Manispaa ya Kinondoni kuwa ni Boniphace Jacob ambaye ni diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema  aliyepata kura 38 wakati mpinzani wake Benjamini Sitta wa CCM akipata kura 20.

Kwa upande wa kiti cha Naibu Meya, Bwana Celestine alimtangaza, Jumanne Amir ambaye ni diwani wa Tandare kwa tiketi ya CUF kuwa  ndiye mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 38 wakati mpinzani wake wa CCM akipata kura 19 huku kura 1 ikiharibika.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply