The House of Favourite Newspapers

UKIANGALIA MBELE UTAYAFURAHIA MAISHA YA UHUSIANO

HELLO marafi ki! Naamini mtakuwa poa kabisa na maisha yanaendelea kwa kasi kama kawaida. Mimi kwa upande wangu ni mzima na ninaendelea na mishemishe zangu vema. Nakukaribisha sana kwenye ukurasa wetu wa Boyfriend & Girlfriend ambao naamini umekuwa msaada kwako kila kukicha. Marafi ki, maisha ni safari yenye mambo mengi sana njiani.

Kuna wakati unaweza kukutana na vitu ambavyo huvipendi. Havikuvutii lakini inakubidi ujitahidi kukabiliana navyo kwa kila hali ili uweze kuvuka na kusogea kwenye hatua nyingine. Ndivyo maisha yalivyo, kila mmoja ana kumbukumbu mbaya katika maisha yake ambazo kwa hakika hapendi kuzikumbuka mara kwa mara.

Kuna mambo yanayoumiza ambayo kwa kawaida binadamu wengi hawapendi kukumbuka machungu. Ndiyo maana binadamu mwenye utashi huyaacha yaliyopita yabaki nyuma na kusonga mbele, mambo ya nyuma yanabaki kuwa somo au daraja la kumfi kisha kwenye eneo jingine.

Hayo ndiyo maisha. Marafi ki zangu, nimeamua kueleza yote hayo kama utangulizi ili iwe rahisi kuzungumzia mada hii. Katika mapenzi, wengi hukutana na wenzi wao ukubwani (nikimaanisha kuanzia miaka 18 na kuendelea). Maisha ya nyuma ya mwenzako si rahisi kuyajua kwa undani. Unaweza kuchunguza baadhi ya mambo kwa lengo la kukusaidia kumjua mwenzako vizuri au kwa bahati mbaya au nzuri akatokea mtu na kukuanikia maisha ya nyuma ya mwenzako.

Kwenye tatizo ni pale ambapo utaelezwa mambo ambayo hutayafurahia. Utaelezwa maisha yake mabaya, uhuni na tabia za hovyo alizowahi kufanya mpenzi wako. Unaweza kumchunguza msichana wako, ukakutana na mtu akakumbia: “Daah! Yule demu hafai kabisa, mtaa mzima huu kauchafua, ameshatembea hadi na wazee.” Je, kwa hali hii unapaswa kufanya nini? Tabia mbaya za wenzako za nyuma zinaweza

kuharibu mapenzi yenu na kuamua kuachana moja kwa moja? Mathalani unaweza kupewa maelezo kwamba mwenzako aliwahi kutoa mimba huko nyuma na mengine mengi ambayo kwa kawaida hukuyajua au hayapendizi tu! Marafi ki zangu, mada hii imezaliwa kutoka kwa msomaji mmoja aliyeuliza kuhusu mpenzi wake.

Alisema: “Kaka Shaluwa, mpenzi wangu nimeambiwa ana tabia mbaya sana. Amewahi kutembea na wasichana watatu ndugu wa familia moja kwa nyakati tofauti. Nasikia alikuwa mlevi sana na watu wote mtaa mzima wanamjua kwa tabia zake mbaya. Naogopa kuolewa naye kutokana na tabia hizo, natamani kumuacha tu. Naomba ushauri wako.” Nilizungumza naye na

kumshauri cha kufanya. Lakini niliona inawezekana wapo wengi wanaokabiliana na jambo kama hili. Wapo wengi ambao wanababaishwa na jambo hili lakini ukweli ni upi?

HISTORIA GANI HASA?

Kimsingi kuna tabia au mambo ambayo hayapendezi kwenye jamii. Kwa kawaida wengi hawapendi kujihusisha na watu wenye tabia au sifa mbaya kwenye jamii. Nimeshafafanua katika kipengele kilichopita hapo juu lakini lengo hasa hapa ni juu ya miendeno mibovu ya kimahusiano na wenzi waliopita. Katika hili yapo mambo ya msingi zaidi kuangaliwa kuliko historia ya nyuma. Twende tukaone.

MWANGALIE KWA UPYA

Ukweli uko wazi marafi ki zangu, ikiwa hukufahamu tabia zake mpaka ulivyosikia

ni wazi kuwa ni mambo ambayo alikuwa akiyafanya huko nyuma. Jambo kubwa kwako kwa sasa ni kumwangalia kwa upya. Chukua uliyoelezwa, yafanyie kazi kwa kuangalia kama bado ana tabia kama hizo. Rafi ki zangu, kukosea nyuma hakumaanishi kwamba ataendelea kuwa yuleyule siku zote. Mwangalie kwa upya alivyo leo. Wiki ijayo tutaendelea mada hii, USIKOSE! Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA kitakachoingia mitaani hivi karibuni

Comments are closed.