The House of Favourite Newspapers

UKIMFANYIA DAWA HII MPENZI WAKO, KAMWE HACHOMOKI!

MNAPOISHI pamoja kwa muda mrefu, huwa kuna migogoro ya hapa na pale inayotokea, ambayo baadaye inaweza kumfanya mtu akamchoka mume au mke wake. Akawa hatamani tena kuendelea kuwa naye, anapomfikiria kichwani mwake anapandwa na hasira, chuki dhidi yake inashindwa kujificha.

 

Mkiwa katika uhusiano wa aina hii, ni rahisi mmoja kati yenu kuanza kuhamishia hisia kwa mtu mwingine wa nje. Kama ni mwanaume, anaweza kuanza kujenga mazoea na mwanamke mwingine wa nje, ambaye atakuwa kila akimfikiria, moyo wake unafurahi, anajisikia furaha na taratibu penzi linaanza kuchipua kati yao.

 

Kama ni mwanamke pia, anaweza kuanza kujenga mazoea na mwanaume mwingine nje, ambaye anapozungumza naye au kuchati naye, moyo wake unafurahi, na penzi linapofikia katika hatua hii, kinachofuatia ni usaliti na penzi kufa kabisa.

 

Unaweza kumfanya mwenzi wako aanze kukufikiria upya, aache kuwaza matatizo mliyopitia, penzi lichanue upya ndani ya moyo wake na amani itawale kati yenu. Unachotakiwa kukifanya ni rahisi sana.

 

MAHITAJI

– Chumvi ya mawe kiasi cha kama nusu kikombe

-Karatasi jeupe

-Kalamu

 

Chukua karatasi jeupe, andika jina kamili la unayetaka awe anakufikiria wewe muda wote, kama ni mumeo au mkeo au mpenzi wako. Baada ya hapo, kunja karatasi mara tano kisha chukua karatasi jingine, weka chumvi ya mawe na karatasi lenye jina la huyo umpendaye, likunje vizuri na hakikisha karatasi limegusana na chumvi.

 

Baada ya hapo tafuta sehemu tulivu, chimba shimo ardhini na weka karatasi lenye chumvi, ukiwa unafukia zungumza maneno ya kumtaka mpenzi wako aanze kukupenda upya, akuwaze wewe tu na akuweke peke yako ndani ya moyo wake.

 

Baada ya hapo fukia vizuri na hakikisha hakuna mtu anayeweza kuja kufukua na kutoa ulichokifukia. Kadiri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele, chumvi itakuwa inayeyuka taratibu na kuliyeyusha pia karatasi lenye jina la umpendaye na utaanza kuona mabadiliko.

KUFURU ya  Steve Nyerere ALIVYOMMWAGIA Pesa Ruby Stejini

Comments are closed.