UKIMGUSA KRISH UTAKIONA CHAMTEMA KUNI

ACHA kabisa! Sexy mama kwenye Bongo Muvi, Irene Uwoya amewaonya wanaomsema vibaya mwanaye wa kiume, Krish kutokana na uzuri wake akiwaambia kuwa wakiendelea watakiona cha mtema kuni.  Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Uwoya alisema anaumizwa mno na watu wanaomsema vibaya Krish kwa maneno yasiyofaa kwa mtoto kwa sababu tu anaonekana mzuri hivyo kuahidi kuwaadabisha wanaofanya hivyo.

“Unakuta mtu anamuombea maneno mabaya Krish, eti kisa nimezaa mtoto mzuri, naomba waache na mtu akitaka kunivuruga, basi amuongelee Krish vibaya,” alisema Uwoya ambaye alimzaa mtoto huyo na aliyekuwa mwanasoka wa Rwanda, marehemu Hamad Ndikumana ‘Katauti’.

Loading...

Toa comment