UKIMYA WA MIAKA 8 WA ICE CUBE UMEILETA ALBUM YAKE MPYA LEO

Rapa na muigizaji maarufu O’Shea Jackson Sr kwa jina maarufu Ice Cube amevunja ukimya wake wa miaka nane baada ya kuja na album yake mpya, ‘Everythangs Corrupt’ yenye nyimbo 16 na aliyomshirikisha rapa mmoja ‘Too short ‘.

 

Akiwa katika mahojiano kwenye Apple music radio Beats 1 na Zane Lawe amefunguka na kusema, “nimejitahidi kuwa mwaminifu kwenye nyimbo zangu.Hawawezi kunidanganya.mwisho wa siku najitahidi kuwaeleza watu ukweli wa kile ninachokiona.Hakuna mtu wa kuomba msamaha kwenye nyimbo zangu.Kama unavyojua nimeongea kila kitu, kila mtu na hata mimi mwenyewe pia nimejiongelea.Nadhani kila penseli inahitaji kuhimarishwa sasa hivi na kila wakati.Nadhani nyimbo zangu ni penseli iliyo imarishwa.”Alimaliza Cube

 

Everythangs Corrupt  ni album ya 10 ya Ice Cube naya kwanza toka mwaka 2010 lakini rapa huyo yupo mbioni kuileta filamu yake ya Last Friday ambayo ni mwendelezo wa Next Friday (2000) na Friday After Next (2002)

 

Album ya Everythangs Corrupt inapatikana kwenye platfomu zote za kuuzia muziki zikiwemo, Apple music, Tidal, Spotify, Amazone na kwingineko.

 

#ISIKUPITE : Harmonize Amkana Wolper Siku Ya Birthday, Alilia PENZI la Sarah

 

Toa comment