The House of Favourite Newspapers

Ukinipa 900…Itapendeza Zaidi

0

Hata uende kwa fundi gani kwangu utarudi tu!” Shaka aliongea kwa kujiamini akifungua simu ya mteja.

Asha hakuwa na namna…kwa pesa aliokuwa ameitenga kwa ajili ya kutengeneza simu yake ilikuwa shilingi elfu kumi na tano tu. Alitumia kila uongo kumdanganya fundi Shaka lakini hakutaka kumuelewa zaidi ya kutaka kuongezewa pesa.

“Sasa jamani fundi…si unifanyie japo kwa shilingi elfu 15?”

“Unacheza kweli wewe! Uliona wapi tachi skrini ya simu ya laki tano ikawekwa kwa shilingi elfu 15?”

Asha alijihisi kijasho chembamba kumtiririka…kila akikumbuka magrupu ya WhatsApp kwenye simu yake…alivyokuwa akipigiwa simu na madanga yake kwa kutumia video call ndiyo alichanganyikiwa kabisa.

“Sawa naenda kukuchukulia pesa yako! Nihakikishie tu itapona kweli?”

“Unauliza mananasi Pwani…we niletee hiyo pesa uone inavyoteleza!”

Asha aligeuza mgongo na kwenda kutafuta kiasi kingine cha pesa ili aweze kutengeneza simu yake…huku nyuma Shaka alijipa uhakika kuwa pesa inaenda kuongezwa hivyo alichofanya ni kuanza kuifungua ile simu harakaharaka…akatafuta tachi skrini ya simu nyingine ambayo ilikuwa na tatizo la tofauti na kumpachikia…

“Kama yeye mtoto wa mjini basi miye ni wa mujini!” Alisema Shaka akimalizia kuifunga ile simu ya Asha…akaanza kuiweka sawa…kwa kuwa haikuwa na namba za siri….kwa bahati mbaya akajikuta amebonyeza eneo la picha na kushuhudia picha za utupu za Asha…

“Ndiyo maana kalikuwa kanang’ang’ania kweli ipone leoleo!” Shaka alijisemea kimoyomoyo akiendelea kufunua picha moja baada ya nyingine…safari hii akili ikamtuma kuingia kwenye eneo la video…napo akashuhudia Asha akila bata na madanga yake…kuna mengine alijirekodi nayo akiwa uwanjani wakilisakata kambumbu…akajitumia zote na kuirudishia kama ilivyokuwa…

“Kanavyoelekea haka katoto katakuwa balaa!”

Shaka akiwa hana hili wala lile katika kuikagua ile simu…Asha akatokea…

“Hee! Kulikoni fundi? Imepona?” Macho yake yalikuwa yametua kwenye mikono ya Shaka na simu yake akajua anamalizia kumtengenezea bila kujua alikuwa akiangalia siri zake…

“Ulivyonipa uhakika kuwa unafuata pesa fasta nikajiongeza…nikachukua pesa yangu mfukoni na kwenda kutafuta skrini tachi na ndiyo hapa namalizia…”

“Loo! Afadhali maana nilikuwa najifikiria tena mpaka nianze kusubiri umalize nitachelewa hata mishe zangu!”

“Kweli kabisa…siku hizi muda una thamani kubwa sana!” Shaka aliongea kinafki na kumgeuzia mgongo Asha…akachukua kifaa na kujifanya akiendelea kuirekebisha…

Harakaharaka akazama WhatsApp ya Asha na kuendelea kukagua meseji moja baada ya nyingine…akaichukua namba ya simu…kitu ambacho Asha hakukijua alielekezwa kwa fundi ambaye hakumjua tabia zake japo alisifika kutengeneza simu za wadada tena warembo….

“Hebu jaribu hapahapa kama ina tatizo niambie!”

Asha aliishika ile simu yake…cha kwanza kabisa aliangalia kama vitu vyake vipo salama kuanzia namba za simu mpaka picha…akajaribisha tachi kama inafanya kazi…

“Hapa sawa kabisa! Ipo freshi!” Akatoa meno nje na mashavu kubonyea kwa mbali…

“Jaribu kupiga au kucheza na hiyo tachi utakavyo!”

“Bwana! Nakuaminia fundi wangu! Umesema unaitwa fundi nani vile?”

“Shaka!”

“Ahaa! Fundi Shaka asante sana!” Asha alitoa kiasi cha ile pesa iliyokuwa imesalia na kumpatia fundi Shaka…

“Kwa ukarimu wako….hii pesa sichukui!”

“Yaani unitese huko mpaka niende kutafuta unasema huchukui? Kwa nini sasa uliniambia nikutafutie hiyo elfu 15?”

“Haaa Asha! Hizo lugha za biashara tu! Nenda ukifika nyumbani nitafute!”

“Haya bwana!” Asha alichukua ile pesa na kuitumbukiza kwenye pochi yake…akamgeukia Shaka…

“Asante sana fundi Shaka!”

Jioni yake…

Akili ya Shaka ilishindwa kabisa kuendana na ukweli wa kile alichokiona mchana kwenye simu ya Asha…haikuwa kawaida yake kufunga eneo lake la kazi saa kumi na moja za jioni…

Alichofanya ni kwenda mpaka kwenye chumba chake kimoja alichopanga maeneo ya Magomeni-Usalama…akajimwagia maji na kukaa kitandani kwa muda…

“Kumbe kuna wateja wangu wengine wanakuwaga na siri kubwa hivi?” Shaka alijisemea chinichini huku akivuta simu yake na kuanza kuangalia picha zote za Asha…

“Hebu ona kama hapa! Kama siyo uchokozi wa wazi ni nini sasa?” Uvumilivu ulimshinda Shaka…akaamua kumpigia simu…

“Nani mwenzangu?”

“Asha mara hii umeshanisahau?”

“Niambie nani? Kama hutaki kata simu kabla sijakubloku?”

“Basi basi mamaaa! Ngoja nakupigia WhatsApp unione sura maana nikikutajia jina napo utasema hunijui!” Harakaharaka Shaka alikata simu na kumpigia kwa WhatsApp kisha akaweka eneo la video…

“Kumbe fundi Shaka muone kwanza!”

“Nilijua tu ukishaniona litakushuka! Vipi simu haijakusumbua tena?”

“Ahh wapi! Yaani fundi kweli wewe niamini!”

“Hata wewe unaonekana fundi kweli!”

“Ningekuwa fundi ningekutafuta?”

“Ila sijamaanisha ufundi huo!”

“Upi sasa?”

“Kwa unavyoonekana tu…kwa ulivyobarikiwa hivyo…mtoto kiuno cha nyigu…utakosaje kuwa fundi kwenye uwanja wa kujidai!”

“Haaa haaa Shaka bwana! Ngoja nikajimwagie maji…nimechoka nimetoka kwenye mizunguko yangu ya kutafuta pesa…”

Shaka hakuwa na jinsi zaidi ya kumsikiliza Asha…wazo lililomjia ni kuhakikisha akitoka tu bafuni akutane na picha yake ya mitego aliyoitoa mchana kwenye simu yake kisha akaandikia…

“Hivi huyu ni wewe?”

Haikuchukua muda…Asha akapiga simu…

“Shaka?”

“Naam mama!”

“Fundi Shaka?”

“Nakusikia…mbona sauti kali hivyo?”

“Nakuomba…tena nisikilize kwa makini? Picha hiyo umeitoa wapi?”

“Kwenye simu yako kwani kuna ubaya mi kuwa nayo?”

“Kuna ubaya tena sana tu! Kumbe ndiyo tabia yako kwa wateja wakileta simu unatoa picha zao…” Asha alimkatia simu Shaka…kwa hofu aliyokuwa nayo akaingia sehemu ya picha zake na kuanza kukagua moja baada ya nyingine…akaingia na sehemu ya video….akajikuta mwili ukimlegea baada ya kushtuka huenda Shaka amegundua siri nyingi zake kupitia picha na video…

“Umefaidika na nini kwa mfano?” Asha aliongea na Shaka kwa mara nyingine…hakuwa Asha yule wa kucheka naye…hasira zilimpanda…

“Tuliza kwanza jazba!”

“Sitaki na nakushtaki nakwambia!”

“Nenda popote!” Shaka alimkatia simu kwa hasira…

Asha alikaa kwa muda akifikiria…akajikuta akijuta kumfahamu fundi Shaka…akampigia kwa mara nyingine lakini safari hii alipoza sauti…

“Hivi nimekukosea nini mpaka uchukue picha zangu? Unapata faida gani sasa?” Asha aliongea kwa sauti iliyoonesha kuwa na kigugumizi…

“Wala hujanikosea kitu sema Asha unapaniki vitu vidogo sana! Nimeshangaa hata kunikatia simu…”

“Noo Shaka! Lazima niwe na hofu…nimejiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu!”

“Upo wapi sasa hivi?” Shaka alimtega…

“Nipo nyumbani kwangu!”

“Najua upo huko wapi? Buguruni, Tabata, Ubungo au wapi?”

“Nipo Kijitonyama huku karibu na stendi ya daladala za Makumbusho….”

“Unaweza kuja Magomeni mara moja?”

“Kufanya nini?”

“Tatizo lako ndilo hilo! Wee njoo au hupendagi bata wewe!”

“Mi na mambo hayo tofauti…kilevi changu siri yangu!” Alisema Asha na moja kwa moja kichwa cha Shaka kikajiongeza na kujua ulevi wake ni ule aliouona kwenye picha…

“Siri yenyewe ndiyo hiyo sasa ninayokuitia!” Shaka alidumbukiza maneno ya kumtega…

“Hutaweza Shaka! Huu muziki mwingine…”

“Nitaweza tu!”

“Shilingi elfu 15 tu ya kutengeneza simu umeng’ang’ania vile!”

“Nitakuongeza mara mbili yake!”

“Hapo sawa! Upo wapi?”

“Nipo Magomeni tena naishi peke yangu!”

“Mhh! Ya kweli hayo?”

“Nikudanganye kwa kipi sasa! Kama huamini njoo uone!”

“Nitumie kwanza pesa ya saluni?” Asha alimtega Shaka…akajaa…harakaharaka akachomoka kitandani na kwenda kumtumia kiasi cha shilingi elfu 10…

“Anza nayo hiyo ukija nitakupa nyingine…”

Asha aliiangalie ile pesa iliyoingia kwenye simu mara mbilimbili…hakutaka kuilazia damu…kwa kuwa hakuwa na plani za kwenda saluni…alijitengeza anavyojua mwenyewe…akaweka vitu vyake muhimu kwenye pochi na kutafuta Bajaj ambayo ilimpeleka mpaka alipo Shaka….

“Karibu na jisikie upo kwako!”

Leave A Reply