The House of Favourite Newspapers

Ukinipa 900… Itapendeza Zaidi-6

ILIPOISHIA IJUMAA: “Hapana!” “Kuna tatizo kukushika kama hivi?” Asha akausogeza mkono wake hadi mashavuni mwa Shaka… Hakuwa Asha yule aliyezoeleka…kilichomleta ni baada ya jana yake kuchezeshwa mechi ya nguvu na Shaka…mechi iliyompagawisha hadi ikamrudisha… “Shaka nimegundua kuwa wewe ni kinyozi wangu!” TAMBAA NAYO UTAKAVYO… SHAKA alimgeukia Asha na kumuangalia mara mbilimbili. “Mi’ na wewe tuna mkataba wa kuwa wapenzi?” “Hapana, lakini…” “Sitaki jibu la hapana… umeona kabisa nimeku-block kwenye simu, ulichofuata hapa ni nini?” “Penzi lako Shaka…ujue usiku wa jana nimekosa kabisa usingizi, ona hata sasa haya nilionayo si mafua, bali kukumisi tu…” Asha aliongea kwa kujiamini huku akikohoa kanakwamba amebanwa na mafua… “Sikiliza…sasa hivi usiku umeingia…ni bora ungetulia nyumbani kwako na kama una familia tulia…” “Shaka hivi nikueleze mara ngapi kwamba ninaishi mwenyewe! Sawa, isiwe tabu kwani sijazoea kubembelezana na wanaume…kama umeamua hivyo sawa, acha nikatafute madanga yangu tu….” Asha aliongea akiwa amejawa na presha…hakuwa Asha yule aliyekuja mwanzoni kwa kubembeleza… Alichokifanya alifungua mlango kwa hasira na kutoka hadi nje ya nyumba aliyokuwa amepanga Shaka na kuondoka zake… “Ndiyo dawa yao! Yaani hata siku tatu hazijaisha tangu nimelala naye, ameshaanza kuniletea mazoea…” Shaka alijisemea kimoyomoyo… Asubuhi yake… “Leo sitaki tena usanii wako, ninachokitaka ni simu yangu ikiwa nzima…” Julius alilalamika mara baada ya kumkuta fundi Shaka ofisini kwake… “Ninajua ila ungeniuliza kwanza sababu ya kutopona hadi sasa?” “Sitaki kujua sababu! Uliniambia ni tatizo dogo na kwamba nikuachie kianzio, nikakupa elfu themanini ya kununua kioo ili ikipona, nimalizie ishirini, haya iko wapi?” Shaka aliinama…ni kweli simu ya Julius ni kati ya simu ambazo alikula kianzio chake na kuiweka pembeni… “Basi nisubiri hapa nikafuatilie kioo chake dukani!” Alisema Shaka huku akiichukua ile simu na kuchomoka…alizubaa mtaa wa pili kwa muda kisha akarudi…

 

“Nimesahau kabisa kumbe lile duka hawafungui leo!” “Fundi Shaka naona tutaelekea kubaya! Ina maana Kariakoo nzima duka la vifaa vya simu lipo moja tu?” “Tatizo siyo duka…ni aina ya kioo chako! Hii ni iPhone 6, kioo chake kwanza ni gharama sana…kwa hiyo pesa yako uliyotoa ni ndogo…” “Unamaanisha niongeze pesa nyingine?” “Kama unataka niende tu duka lolote niongezee pesa… lakini ujue kabisa bei za vioo ni kuanzia laki moja na nusu, hiyo themanini niliokwambia ni kwa magumashi tu…” alijitetea Shaka na kumfanya Julius kuzama mfukoni na kuongeza kiasi cha pesa… Kitendo cha kumkabidhi tu kiasi cha pesa…. akatokea mrembo mmoja na kumkumbatia Julius akiwa na furaha…ngozi yake ya maji ya kunde na udogo wa eneo la kifuani mwake ukichangia na lipsi zake nene, ukamfanya
Shaka aduwaye… “Umefuata nini hadi huku?” Alisema Julius… “Jamani mume wangu! Mara hii umeshasahau kama hiki ni kipindi cha kuelekea sikukuu na wewe ndiyo umeniachia pesa ya kuwafanyia manunuzi watoto…” “Ahh! Uzee nao huu! Nimeshakumbuka, nilijua utaenda maduka mengine siyo Kariakoo!” “Ni Kariakoo mume! Haya na wewe umefuata nini huku?”

 

“Si unaikumbuka ile iPhone yangu iliyodondoka kipindi kile na kuharibika kioo! Niliileta kwa fundi huyu hapa! Sasa hapa nilipo ninahangaika kweli na hii simu nyingine, ninapata tabu hata kuitumia…” Maongezi ya Julius na mumewe yalikuwa marefu kidogo na kumfanya Shaka aendelee kuwaangalia… muda wote huo akili yake ilishavutika kwa mke wa Julius… katika maisha yake hakuwahi kukutana na mwanamke mwenye shepu yake na mwenye vigezo vya aina ile…

 

“Fundi?” Julius alimuita Shaka… “Naam bosi wangu!” “Nimeshapata msaada hapa! Ngoja nirudi ofisini….mke wangu huyu hapa atarudi nayo na ninampatia na kiasi chako kilichobaki…” Moyo wa Shaka ni kama ulishukuru kwa mtego huo kufyatuliwa…akajihisi kuwa na amani… “Usijali bosi…nitampatia na kama kukiwa na tatizo lingine utanijulisha…” “Sawa namba yako ni ipi tena?” Julius alimsogelea Shaka na kubadilishana naye namba za simu… “Baadaye basi!” “Sawa bosi wangu!” Shaka hakutaka hata kuuliza mke wa Julius anaitwa nani zaidi ya kumuitikia harakaharaka ampe upenyo… “Karibu ukae…karibu!” “Unafikiri mkaaji basi! Bado sijamalizia kufanya manunuzi… naomba niende duka la mtaa
huo wa Swahili kisha nitarudi…si utakuwa umeshamaliza?”

 

“Nenda tu usiwe na shaka kama lilivyo jina langu!” Shaka alijifagilia… “Unaonekana mcheshi sana wewe!” “Haaa…haaa… fundi bwana! Nishikie basi hii mizigo yangu niwekee hapo ndani ya ofisi yako!” Shaka alifanya kama vile ni hausiboi…aliichukua ile mizigo ya mke wa Julius na kuingiza ndani ya ofisi yake harakaharaka… “Kingine?” “Kingine ninarudi sasa hivi!” Mke wa Julius alionesha tabasamu na kutaka kuondoka… hatua mbili mbele, Shaka akamuita… “Samahani lakini!” “Bila samahani!” “Ninatoka mara moja, nakwenda kutafuta kioo cha simu ya mumeo, sasa hapa lazima nifunge kwa muda kwa sababu sina msaidizi leo…”

 

“Jamani fundi si ungeniambia kabla sijaweka mizigo yangu?” “Hapana! Nilichotaka kukwambia, naomba namba yako ya simu kama tutapisha utanipigia si unajua Kariakoo hiihii, mi’ naenda mtaa huu wewe ule?” Maneno hayo yalimuingia mke wa Julius bila kuelewa ujanja aliotumia Shaka wa kuchukua namba yake ya simu…akajikuta akimpatia namba ya simu… “Nisevu jina gani sasa?” “Andika mke wa Julius mi’ nasevu fundi!” “Kama umeamua hivyo sawa!” “Unaweza kuniambia pia unapenda nikusevu kwa jina gani?” “Basi andika vyovyote tu ili ukiitafuta usipate shida!” Mke wa Julius alisevu anavyojua…akaagana na Shaka kila mmoja akaenda upande wake… Haikupita dakika ishirini mke wa Julius akawa wa kwanza kumtafuta Julius…

 

“Umesharudi ofisini kwako?” “Nipo ofisini na simu yako tayari ninayo ila sijui nimesahau vipi yaani?” “Kuna tatizo tena?” “Kuna mkanda wa kamera wa ndani kwa ndani…ujue hii simu niliifungulia nyumbani sasa kuna baadhi ya vifaa nimeviacha hukohuko!” “Hebu nakuja hukohuko ofisini!” Shaka alikata simu akicheka kimoyomoyo! Hakuna cha mkanda wa kamera aliokuwa ameusahau nyumbani zaidi ya kuanza kumfanyia mitego mke wa Julius… dakika chache akawa amefika… “Umenishtua sana! Ufuate basi nipo tayari kukusubiri maana ninavyomjua Julius hawezi kunielewa kabisaaa… nikirudi mikono mitupu!” “Hakijaharibika kitu…kwani mnaishi wapi?” “Tunaishi Ubungo au…kwa nini nisimpigie Julius kwa kuwa ameniambia anarudi kazini ili akirudi aipitie si utakuwa umeshachukua huo mkanda na kuurudishia?” Mke wa Julius alihoji…

 

 

“Ngoja nikupe wepesi! Umesema unaishi Ubungo?” “Ndiyo!” “Mi’ ninaishi Magomeni, kwa nini tusiongozane samahani lakini…yaani tuende hadi kwangu nikufungie haraka kisha uende kwa kuwa ni njia hiyohiyo ya kwenda Ubungo…” Mke wa Julius alifikiria mara mbilimbili akaona ni sawa… “Haichukui muda lakini?” “Sijui hata nikuambieje…ni kitendo cha dakika chache tu!” Mama Julius alikubaliana na Shaka…wakasaidiana mizigo… Shaka akafunga ofisi yake moja kwa moja kisha safari ya kuelekea kwake ikaanza… kichwani alijihakikishia hawezi kumuacha hivihivi huko aendapo! Je, nini kiliendelea? Usikose Ijumaa kwenye Gazeti la Ijumaa

Comments are closed.