UKITAKA KUANZISHA HUDUMA ZA ‘LAUNDRY’, FUATA HATUA HIZI RAHISI

 

Udobi ni kazi ambayo imezoeleka kwamba inafanyika kikawaida kabisa. Wasichokijua wengi ni kwamba, unaweza kujikwamua kiuchumi na kupata mafanikio makubwa kama utaamua kufanya kazi ya udobi kitaalamu (laundry). Udobi unaozungumziwa hapa, siyo ule wa kufua mashati mawili na suruali kwa mkono, kisha unayaanika na baadaye kuyapiga pasi, au kufua suti na kunyoosha kwa mkono, hapana! Udobi unaozungumziwa hapa ni ule wa kutumia mashine.

Habari njema ni kwamba unapofikiria kuanzia biashara hii, tambua kwamba kampuni ya uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mahotelini, majumbani na viwanda vidogo ya Uni Industries, itakuwa nawe bega kwa bega kukurahisishia upatikanaji wa mashine zote zinazotakiwa kwa ajili ya kufungua huduma ya laundry.

“Vifaa vya muhimu vinavyotakiwa kuwa navyo, kwanza unatakiwa kuwa na chumba kwa ajili ya kuweka mashine zako, mahali ambapo ndiyo kazi ya udobi itakapokuwa inafanyika. Chumba kinapaswa kuwa kisafi, chenye hewa nzuri na chenye nafasi ya kutosha. Pia unatakiwa kuwa na mashine ya kufulia na hapa tunazo za aina nyingi zinazotofautiana ukubwa.

“Zipo mashine ndogo lakini zipo nyingine kubwa kutegemeana na matumizi yako. Hizi kitaalamu zinaitwa Semi Commercial Washer. “Pia kuna mashine nyingine kwa ajili ya kukausha nguo, kwa kitaalamu zinaitwa Semi Commercial Dryer, uzuri wa hizi ni kwamba zinakausha nguo haraka bila kutegemea jua, na pia mashine nyingine muhimu ni pasi ya kisasa (roller ironer). Hii itakusaidia kunyoosha mashuka, mataulo au nguo nyingine nyingi ndani ya muda mfupi,” alisema Roscoe Bremer, Meneja wa Kanda wa Uni Industries.

Bremer aliongeza kwamba mashine zote hizi zinapatikana kwa bei rahisi kwenye maduka ya Uni Industries yaliyosambaa kuanzia hapa jijini Dar es Salaam, Zanzibar, Kenya, Uganda na Rwanda. “Pia tunavyo vifaa vingine kwa ajili ya mahitaji kuanzia ya jikoni, mahotelini, supermarket na mashine za kufulia, majiko ya kupikia keki, majiko ya kuona mikate, kukata mbogamboga na matunda, kutengenezea juisi na kadhalika. Bidhaa zetu zina kiwango cha kimataifa na mteja anaponunua, anakuwa na uhakika wa fedha zake kwa kipindi kirefu.

“Lakini pia tunavyo vifaa vingine kama majokofu ya kisasa ya ukubwa tofautitofauti, vifaa vya kusambazia vyakula kwenye sherehe na shughuli mbalimbali (catering services), vifaa vya supermarket kama ‘shelves’ za kisasa, samani za ndani na vingine vingi.” Kwa mahitaji ya vifaa vingine vingi vya kisasa, tembelea maduka ya Uni Industries yaliyopo Staywell Complex, plot 1720, Haile Sellasie Road, mkabala na Marrybrown, Namanga jijini Dar es Salaam na Forodhani, Zanzibar.

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0681 111 999 au 0766 075 031 au kwa barua pepe [email protected]. Pia unaweza kutembea website yao kwa kubofya www.uni-eastafrica.com. Wahi sasa ili uwe miongoni mwa watu wanaokwenda na wakati kwa kumiliki vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu.

Toa comment