The House of Favourite Newspapers

UKITAKA KUFUNGUA HUDUMA YA CARTERING, FUATA HATUA HIZI RAHISI

 

Miongoni mwa huduma ambazo zimekuwa kimbilio la wajasiriamali wengi, ni huduma ya kutoa huduma ya vyakula kwenye sherehe au mikutano (cartering services) na wengi wanaofanya shughuli hii, wamepata maendeleo makubwa.

Kutokana na kulipa kwa biashara hii, wajasiriamali wengi wanashawishika kuingia kwenye biashara hii lakini kwa bahati mbaya, wengi huwa hawajui hata ni wapi pa kuanzia.

Habari njema ni kwamba unapofikiria kuanzia biashara hii, tambua kwamba kampuni ya uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mahotelini, majumbani na viwanda vidogo ya Uni Industries, itakuwa nawe bega kwa bega kukurahisishia upatikanaji wa vifaa vyote vinavyotakiwa katika biashara ya cartering.

“Jambo la kwanza ambalo mtu anayetaka kuanzisha biashara hii anapaswa kulifanya, ni kutafuta wapishi wazuri wanaoweza kupika vyakula mbalimbali kwa ufanisi wa hali ya juu. Jambo la pili, ni mjasiriamali kuwa na vifaa muhimu vya kuhifadhia vyakula na kuandalia, tayari kwa watu kujisevia.

“Na hapa ndipo umuhimu wa Uni Industries unapoonekana, tunavyo vifaa bora kabisa na vya kisasa, vyenye mwonekano utakaomfanya anayetaka kula, kufurahia chakula.

“Tunayo mabakuli makubwa au kwa kitaalamu ‘chafers’ ya aina mbalimbali, kuanzia ya duara na ya pembe nne yenye uwezo wa kukifanya chakula kiwe cha moto muda wote yakiwa na stendi zake kwa ajili ya kuwekea mezani, tunayo mabirika ya kahawa (cofee urns), juice dispencer na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya kazi hiyo kama sahani, mabakuli na kadhalika.

“Pia mjasiriamali anatakiwa kuwa na timu ya watu wa kutoa huduma ukumbini, ambao wanapaswa kuwa na sare maalum na nadhifu, na kingine muhimu, mjasiriamali anapaswa kuwa na uhakika wa usafiri mzuri wa kupeleka vyakula ukumbini na kurudisha vyombo. Hayo ndiyo mahitaji makuu yamsingi ingawa yapo mengine madogomadogo.

“Mjasiriamali akifika kwetu, mbali na kujipatia vifaa hivyo kwa bei nafuu, pia tutampa ushauri wa namna nzuri ya kupanga vyombo ukumbini na kuendesha biashara yake kwa faida,” alisema Roscoe Bremer, Meneja wa Kanda wa Uni Industries na kuongeza:

“Bidhaa zetu zote zinatengenezwa kwa ubora wa kimataifa, tunavyo vifaa kutoka kwa washirika wetu, MacAdams, IPSO, Fooderv Solutions na kadhalika, yanayosifika kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu duniani kote.

“Maduka ya Uni Industries pia yamesambaa kuanzia hapa jijini Dar es Salaam, Zanzibar, Kenya, Uganda na Rwanda na hii ni uthibitisho mwingine kwamba ubora wetu ni wa kimataifa.

“Mbali na vifaa vinavyotakiwa ukitaka kuanzisha biashara ya cartering, pia tunavyo vifaa vingi kwa ajili ya mahitaji kuanzia ya jikoni, mahotelini, supermarket na mashine za kufulia, majiko ya kupikia keki, kukata mbogamboga na matunda, kutengenezea juisi, kuoka mikate na kadhalika. Bidhaa zetu zina kiwango cha kimataifa na mteja anaponunua, anakuwa na uhakika wa fedha zake kwa kipindi kirefu.

“Lakini pia tunavyo vifaa vingine kama majokofu ya kisasa ya ukubwa tofautitofauti, mashine za kufulia, vifaa vya supermarket kama ‘shelves’ za kisasa, samani za ndani na vingine vingi.”

Kwa mahitaji ya vifaa vingine vingi vya kisasa, tembelea maduka ya Uni Industries yaliyopo Staywell Complex, plot 1720, Haile Sellasie Road, mkabala na Marrybrown, Namanga jijini Dar es Salaam na Forodhani, Zanzibar.

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0681 111 999 au 0766 075 031 au kwa barua pepe [email protected]. Pia unaweza kutembea website yao kwa kubofya www.uni-eastafrica.com. Wahi sasa ili uwe miongoni mwa watu wanaokwenda na wakati kwa kumiliki vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu.

Comments are closed.