The House of Favourite Newspapers

Ukraine Yagoma Kusalimu Amri Kwa Urusi

0


Mshauri mkuu wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema Ukraine haipo tayari kusalimisha eneo lake lote kwa Urusi kama nchi hiyo inavyoshinikiza.

Alexander Rodnyansky ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha BBC Radio 4’s World at One na kueleza kuwa shinikizo la Urusi ni kubwa lakini hawapo tayari kwa hatua hiyo.

“Ni wazi kwamba hawawezi kuendeleza vita hivi kwa miaka mingi na ari yao ipo chini hata hawawezi kuendelea kuvipa vikosi vyao vifaa kuendelea na mapigano,” alinukuliwa Zelensky.

Rodnyansky, ambaye pia ni profesa msaidizi wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alisema Ukraine haitasilimisha uadilifu wa kieneo.

“Ukiwauliza watu wanaoishi katika maeneo haya, hawataki kuishi Urusi. Je, tunawezaje kuwaacha? Achilia mbali wazo zima la kuikata nchi yetu?” alisema Rodnyansky.

Akaendelea kwa kupendekeza kuwa toleo halisi zaidi la mkataba wa Budapest ambalo liliipa Ukraine hakikisho la usalama – lingekuwa muhimu kufikia amani.

“Mkataba wa Budapest ulipaswa kuhakikisha usalama wetu kwa malipo ya kuacha silaha za nyuklia katika miaka ya 90.

“Inabidi iwe kitu kama hicho ambapo hatua zingebainishwa, ni nchi gani hasa zingechukua hatua kwa njia gani ikiwa usalama wako unatishiwa.”

Lakini alionya kwamba uwezekano wa kuhusika kwa nchi za Nato katika mapatano kama hayo itakuwa “suala tete”.
“Ndio maana mazungumzo sio rahisi, kwa sababu haungependa kuanzisha Kifungu cha 5, kimsingi, kuvuta Nato yote kwenye mzozo na Urusi.

“Hiyo ndiyo (ambayo) nchi za Nato hazitaki kutokea na ndiyo maana mazungumzo bado yanaendelea.”

Leave A Reply