The House of Favourite Newspapers

Ukraine Yakanusha Kulilipua bomba la Gesi ya Urusi la Nord Stream

0

Ukraine imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulio lililotokea mwezi Septemba mwaka jana kwenye mabomba ya Nord Stream, ambayo yalibeba gesi ya Urusi kwenda Ulaya.

Ufafanuzi wa Ukraine unakuja baada ya ripoti ya gazeti la New York Times, ambayo inawataja maafisa wa kijasusi wa Marekani ambao wanasema kundi linalounga mkono Ukraine ndilo linalaumiwa.

Katika ripoti tofauti, vyombo vya habari vya Ujerumani vinasema wachunguzi wanaamini walitambua mashua iliyotumiwa kutega vilipuzi.

Usafirishaji wa gesi kupitia bomba ulikuwa umesitishwa kabla ya milipuko hiyo.

Urusi ilifunga bomba la Nord Stream 1 ,mwezi Agosti mwaka jana, ikidai linahitaji matengenezo. Nord Stream 2 haijawahi kuwekwa kwenye huduma.

Sababu kamili ya milipuko iliyotokea mwezi Septemba tarehe 26 ambayo iligonga mabomba ya gesi asilia haijulikani, lakini inaaminika kuwa walishambuliwa.

Moscow imezilaumu nchi za Magharibi kwa milipuko hiyo na kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwachunguza.

Viongozi wa Nato na nchi za Magharibi wameacha kuishutumu Urusi moja kwa moja, ingawa EU imesema hapo awali Urusi inatumia mabomba yake ya gesi kama silaha dhidi ya Magharibi.

#EXCLUSIVE: RAHISA AFICHUA UJAUZITO wa PATRICK, AANIKA SMS za NIFFER, AMTUMIA SALAMU HIDAYA NJAIDI..

Leave A Reply