The House of Favourite Newspapers

Ukraine Yapungua Idadi ya Wanadiplomasia Katika Ubalozi wa Iran Nchini Humo

0
Ndege za kivita zisizokuwa na Rubani zinazotumiwa na Urusi kutoka Iran

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kupunguza idadi ya wanadiplomasia katika Ubalozi wa Iran nchini humo kufuatia kutunguliwa kwa ndege za kivita zisizo na Rubani zinazofanya mashambulizi nchini humo na vikosi vya Urusi ambazo imebainika kuwa ndege hizo zimetengenezwa na Iran na kutolewa kama msaada Urusi.

 

Zelensky amesema ameamua kufanya hivyo kama ishara ya kutopendezwa na uhusiano wa nchi yake pamoja na Iran kwani nchi yake imekuwa ikishambuliwa na ndege hizo zisizokuwa na Rubani kutoka Urusi chini ya msaada wa Iran taifa ambalo lilitangaza kutofungamana na upande wowote kwenye vita hiyo.

Mashambulizi yanaendelea nchini Ukraine kutoka vikosi vya Urusi

Akihutubia Taifa jioni ya Ijumaa Zelensky alisema:

“Leo Warusi walitumia ndege za kivita zisizokuwa na Rubani ambazo zimetengenezwa nchini Iran na kushambulia mikoa ya Dnipropetrovsk pamoja na Odesa. Nimeiagiza Wizara ya Mambo ya Nje kushughulikia suala hili kwa uzito wake.”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

Naye Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ukraine Oleg Nikolenko ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa kutokana na usambazaji wa silaha za Iran kwa nchi ya Urusi kama Wizara tumetangaza kulifanyia kazi suala hili na Ubalozi wa Iran ikiwemo kupunguza baadhi ya Wanadiplomasia hapa Kyiv.”

 

Mapema wiki hii Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza iliiunga mkono Ukraine kuwa mashambulizi yake dhidi ya Urusi yalikuwa yakizuiliwa na ndege za kivita zisizokuwa na Rubani za Urusi ambazo zimetengenezwa na Iran.

Leave A Reply