UKWAJU HUZUIA SARATANI, HUPONYA NOYO, NYONGO

TUNDA la ukwaju lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

FAIDA YA JUISI YA UKWAJU

Ukwaju ni chanzo kizuri cha viuasumu mwilini ‘antioxidants’ ambavyo huzuia saratani (cancer) pia ni chanzo cha Vitamini B na C vilevile “carotentes”. Ukwaju hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo. Hulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni. Ukwaju husaidia myeyusho na mmeng’enyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa na husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders).

Ukwaju pia husaidia kurahisisha choo (laxative), hupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo. Ukwaju husaidia ngozi kuwa nyororo, vilevile husaidia kupona ngozi baada ya kuungua au yenye vidonda.

Ukwaju husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo). Lakini kati ya faida nyingine nyingi za virutubisho na kiafya za ukwaju, ni kwamba unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni, kutibu matatizo ya nyongo, ukwaju unapunguza pia cholesterol mwilini, unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema. Unasaidia kutibu uvimbe.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU

Nunua ukwaju wako, unapatikana kwa wingi sana sokoni na kwenye supermarket. Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu.

Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe, andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juisi yako kwa uangalifu zaidi. Weka sukari au asali kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata testi, weka juisi yako kwenye jokofu (fridge) ili ipoe tayari kwa kunywa.

Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwa sababu una faida nyingi kiafya kama tulivyoainisha hapo juu, hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla Kwa hiyo siku nyingine unapoenda kufanya manunuzi ya vyakula hakikisha unanunua na ukwaju.

Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna vifundo vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi. Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu wanakula ili kupata virutubisho na faida za kiafya za ukwaju.

Ukwaju una ladha faluni ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri unavyokua na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.

Ukweli umeusoma hapa na kujua kuwa kula ukwaju au bidhaa zitokanazo na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema kama tulivyoeleza hapo juu. Sambamba na hayo, mtu atumie juisi ya ukwaju daima angalau anywe mara tano au hata sita kwa wiki angalau glasi mbili.


Loading...

Toa comment