visa

Ukweli Harmo kumtema Sarah

HABARI inayofukuta huko mitandaoni zinadai kwamba mkali wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ au Harmo amemwagana na mkewe Sarah, lakini Risasi Mchanganyiko limezama mzigoni na kuibuka na ukweli.  Awali, vyanzo mbalimbali vililieleza Risasi Mchanganyiko kuwa, wawili hao wameshaachana na kumwaga vithibitisho vyao.

“Wewe angalia hata kwenye mitandao siku hizi, mara ya mwisho ni lini kuona Harmo amemposti Sarah? “Kila mtu ana mambo yake kwa sasa na ndio maana unaona hata kwenye shoo hawaambatani. Zamani ilikuwa Harmo anapokwenda popote kupafomu, lazima Sarah naye aende,” kilimwaga ubuyu chanzo makini.

Katika kusaka ukweli wa mambo, Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kuzungumza na rafiki wa karibu wa Harmo ambaye aliomba hifadhi ya jina, lakini akaeleza kuwa wawili hao hawajaachana.

“Hawajaachana bwana, wamebadili tu aina ya maisha. Sasa hivi hawataki kuambatana kama ilivyokuwa zamani, lakini pia uongozi umembadilishia mipango kwa kutoambatana naye katika shoo,” alisema rafiki huyo.

Kama hiyo haitoshi, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta meneja wa Harmo, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ hivi karibuni kufanya naye mazungumzo marefu ya kazi yake ambapo pia, alifunguka kuhusu suala la Sarah kutoambatana na Harmo. Risasi: Kwa nini siku hizi Sarah haongozani na Harmo kwenye kazi zake?

Mjerumani:

“Kila mtu ana maisha yake, hili suala ni la kifamilia. Sarah anashirikishwa kwenye mambo ambayo anapaswa kuyajua kwa sababu sisi kama uongozi, hatutaki kuingiza biashara na mahusiano. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba kuna maeneo ambayo anatakiwa awepo na sio kila mahali, nadhani hii ndiyo sababu watu wengi wanaona Sarah na Harmo hawaongozani kila mahali pamoja.

Harmo na Sarah walianza uhusiano wao tangu angali msanii huyo alipokuwa Wasafi Classic Baby (WCB) ambapo inaelezwa kuwa wawili hao walikwenda kuposana nchini Italia, nyumbani kwao mrembo huyo kisha baadaye kufunga ndoa jijini Dar.

STORI :Memorise Richard, Risasi
Toa comment