The House of Favourite Newspapers

Ukweli Kigogo wa Polisi Aliyeuawa Kinyama Dar

0

STORI: GLADNESS MALLYA NA MAYASA MARIWATA | IJUMAA WIKIENDA

DAR ES SALAAM: Hali inazidi kuwa mbaya kufuatia ongezeko la matukio ya uvamizi, ujambazi na mauaji yanayoendelea nchini, lakini tukio la kuuawa kwa kigogo wa Jeshi la Polisi Tanzania (PT) aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Uvinza mkoani Kigoma, Amedeus Ernest Marenge, linatisha zaidi.

Jeneza lenye mwili wa marehemu likipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa.

Marenge aliuawa kikatili na watu wasiojulikana hivi karibuni nje ya nyumba yake huko Kinyerezi-Kanga jijini Dar ambapo ndugu na wanafamilia walilieleza Wikienda kilichomponza hadi  kakutwa na umauti vinginevyo angekuwa anadunda tu mtaani.

Kwa mujibu wa majirani waliozungumza na Wikienda, Marenge alirejea nyumbani kwake akitokea kutafuta msosi, maana haishi na familia kwenye nyumba hiyo ndipo akakutwa na tukio hilo.

Ilisemekana kwamba, wakati anarejea aliwakuta walinzi wake wametekwa na wauaji hao hivyo alisimamisha gari, akashusha kioo na kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea.

“Hapo ndipo alipofanya kosa maana wale jamaa waliachana na walinzi hao, wakamvamia na kumshambulia kwa mapanga hadi akafa,” alisema mmoja wa majirani hao aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, kaka wa marehemu, Pius Lucas Marenge alieleza kuwa, tukio hilo la kuuawa kinyama kwa ndugu yake limeacha sintofahamu katika familia yao.

Alisema Marenge aliuawa na watu wasiojulikana kwa kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kuchukua vitu mbalimbali alivyokuwa navyo kwenye gari, tukio ambalo lilijiri usiku wakati Marenge akielekea nyumbani kwake kulala.

“Amedeus (Marenge) alikuja Dar kwa ajili ya harusi ya binti yake ambayo sherehe ya kuagwa ilifanyika Mei 11, mwaka huu na harusi ikawa Mei 14.

“Kwa kweli harusi iliisha vizuri kwa sababu watu walifurahia sana. Lakini siku mbili baadaye ndipo furaha ikageuka simanzi kuu kwani mdogo wangu aliuawa kikatili.

“Hivyo niseme tu kuwa, kama asingekuja kwenye sherehe ya mwanaye au kusingekuwa na harusi, basi asingekutwa na balaa hili. Hicho ndicho kilichompoza mdogo wangu,” alisema kaka huyo wa marehemu.

OCD Amedeus Ernest Marenge enzi za uhai wake.

Akizungumza katika ibada ya kuagwa kwa mwili wa marehemu Marenge iliyofanyika kwenye Kota za Polisi Buguruni, Dar, Ijumaa iliyopita, Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lucas Mkondya alieleza kuwa, wamebaki kwenye mshtuko mkubwa usioelezeka hivyo wanaendelea kuwasaka wauaji usiku na mchana.

Alisema kuwa, baada ya siku chache watawapata wahusika na sheria itafuata mkondo wake.

“Msiba huu uwe kichocheo cha kuwafi chua wahalifu tunaoishi nao kwenye nyumba au mitaani kwetu, toeni taarifa kwa Jeshi la Polisi na sisi tunawahakikishia tutawakamata wahalifu wote maana tumefi kia hatua nzuri na siku chache tutawapata,” alisema Kamanda Mkondya.

Marenge ameacha mjane mmoja na watoto watatu na mwili wake ulisafi rishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yaliyofanyika Jumamosi katika Kijiji cha Kirua-Vunjo, Moshi Vijijini.

Enzi za uhai wake, Marenge aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi (OC-CID) wa Kibaha mkoani Pwani kabla ya kuhamishiwa Uvinza, Kigoma alikokuwa akiendelea na kazi hadi alipofi kwa na umauti

Leave A Reply