The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ukweli Kuhusu Wanafunzi Kukimbia Kipimo Kipya cha Corona

0

VIDEO inayosambaa mtandaoni inaonyesha madai ya uongo ya wanafunzi wa shule wakiwa wanakimbia kuchomwa chanjo ya corona kwa lazima.

 

 

Ukweli ni kwamba video hiyo ilipigwa miezi saba kabla hata kisa cha kwanza cha mgonjwa wa corona kuripotiwa nchini China na kabla hata ya chanjo yoyote ya corona kuanza kutengenezwa.

 

 

Video hiyo inaonyesha watoto wakikimbia kwenye korido huku wengine wakiruka kutoka kwenye madarasa na wengine wakikimbia na mabegi yao. Mtumiaji mmoja wa Facebook alisema watoto hao walikuwa wanakimbia kuchomwa chanjo ya corona.

 

 

Lakini ukweli ni kwamba video hii ilitumika na TV ya Nigeria, Daily Trust, Mei 26, 2019, ikisema kulikuwa na mlipuko wa mabomu ya kutoa machozi katika Shule ya Sekondari ya Community iliyopo Port Harcourt, kusini mwa Nigeria.

 

 

Kituo cha TV cha Abuja kinasema kijana mmoja mwenye miaka 17 alikuwa amebeba mikebe ya mabomu ya gesi na kuwaonyesha wanafunzi wenzake.

Leave A Reply