The House of Favourite Newspapers

Ukweli wa Viumbe Waishio Angani-9

0

aliensETWamarekani wadai Obama shujaa wa kupambana na Aliens

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Wiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikielezea namna ambavyo viumbe hawa wa ajabu waishio angani, Aliens wanavyohusishwa na Eneo la Area 51 lililopo katika Jimbo la Nevada nchini Marekani na jinsi walivyoweza kutengeneza ndege zenye muonekano wa sahani ambazo kwa sasa zinatengenezwa na Wamarekani. SASA ENDELEA…

Kuna andiko la siri linalodai kwamba Rais wa 40 wa Marekani ambaye alikuwa ni mwanachama wa asasi ya siri inayokwenda kwa jina la Knights of Malta na mwenye damu ya kifalme, Ronald Wilson Reagan aliyekuwa rais wa nchi hiyo kati ya mwaka 1981 hadi 1989, mara kwa mara alikuwa akizungumzia namna gani dunia nzima itaweza kuungana endapo patakuwepo na kitisho cha uvamizi wa viumbe hawa wa Aliens.

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Septemba 21, 1987, Reagan aliyefariki dunia 2004 alikaririwa akisema:

“Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyonayo hivi sasa, mara kwa mara tunasahau ni kiasi gani binadamu tumeungana. Huenda tunahitaji kitu kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakachotufanya sisi kuweza kutambua umoja huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha viumbe hawa (Aliens) kutoka nje ya sayari yetu ya dunia.”

Kama hiyo haitoshi, Mei 5, 1988 ndani ya Ikulu ya Marekani (White House), kwenye chumba kilichojaa waandishi wa habari, Reagan alikaririwa tena akisema:

“Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba, itakuwaje kama sisi sote hapa duniani tukagundua kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka nje ya dunia yetu… nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je, si mara moja tu tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho?”

Wazo hili la kuwa kuna kitisho kutoka nje ya dunia yetu, nje ya mfumo wetu wa jua, rais huyo alikuwa akitaja kitisho cha viumbe hao mara kwa mara wakati na baada ya uongozi wake.

Kwenye mkutano wa Bilderberger, Evians, Ufaransa mwaka 1992, Henry Kissinger, mwanasayansi na diplomasia wa Kimarekani naye alikaririwa akisema:

“Leo hii Marekani itakasirishwa endapo Umoja wa Mataifa utaingia Los Angeles (Marekani) kutuliza ghasia. Lakini kesho watafurahia kitu hicho! Hii ni kweli hasa endapo wataambiwa kuna kitisho kutoka nje ya sayari yetu kinachotishia uhai wetu.

“Itakuwa hivyo kwa watu wote wa dunia ambapo wataomba msaada wa kupambana na kitisho hicho. Kitu kimoja ambacho kila mtu anakiogopa ni kile ambacho hakifahamiki. Walimwengu watakapoletewa kitisho hicho, haki zao za msingi wataziachia na kuzikabidhi kwa serikali ya dunia ambayo itawahakikishia usalama wao.” Wakati anaingia madarakani mwaka 2008, rais wa sasa wa Marekani, Barack Obama, Wamarekani walidai wamepata shujaa mwenye uwezo wa kuliokoa taifa hilo kwenye shambulizi la viumbe wa Aliens wasiojulikana kutoka kwenye sayari nyingine. Asilimia 72 ya wananchi wa taifa hilo waliamini juu ya kuwepo kwa viumbe hao na uwezekano wa kutokea kitisho hicho.

Kwenye miaka ya karibuni, neno ‘UFO’ (Unidentified Flying Object) limechukua kasi kwenye vyombo vya habari, hasa nchi za Magharibi, Asia na Marekani. Vyombo hivyo (ndege) vina muonekano wa duara lakini pia vinaweza kuwa na umbo lingine tofauti na hilo kama tulivyoona wiki iliyopita.

Taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na maelezo ya watafiti katika suala hilo ni kuwa UFO hutumika kama chombo cha anga cha kusafiria kwa viumbe hao wasiojulikana kutoka sayari ya mbali. Lakini tabia yake ni tofauti sana na vyombo vyetu vya anga.

Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.

Leave A Reply