The House of Favourite Newspapers

Ulimmisi Solo Thang? Huyu Hapa!


MAKALA: ERICK EVARIST |RISASI JUMAMOSI| RISASI VIBES

KWA kizazi kile kilichokuwa na ufahamu wa muziki miaka ya 2000, jina la Solo Thang si geni, lilikuwa kubwa sana.

Jina lake halisi anaitwa Msafiri Kondo ni miongoni mwa mastaa wakubwa wa Hip Hop kuwahi kutokea Bongo. Solo ni miongoni mwa wasanii watatu walioitendea haki ngoma ya Mtazamo ambayo wakati inatoka, ilikuwa ni kama wimbo wa taifa.

Solo Thang.

Wakali wengine waliosikika humo ni Joseph Haule ‘Profesa Jay’ na Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ambaye ndiye aliyekuwa akiimiliki ngoma hiyo. Profesa na Solo walipewa kolabo.

Mchanganyiko wao ulikuwa na heshima kubwa. Ni moja kati ya kolabo kali zilizowahi kutokea nchini. Amefanya mambo mengi makubwa, kisha akatokomea majuu.

Joseph Haule ‘Profesa Jay’

Mikito Nusunusu imepiga naye stori moja kwa moja kutokea nchini Ireland, huyu hapa:

MIKITO NUSUNUSU: Umekuwa kimya kidogo, vipi kimya chako kina mshindo nini?

SOLO THANG: Siyo kwamba nipo kimya kihivyo, nimeachia ngoma kama wiki mbili zilizopita. Inaitwa Uchu. Tayari nimeanza kupata mrejesho, inafanya vizuri.

MIKITO NUSUNUSU: Yeah! Labda kwa kuwa bado haijapata sana air time, umefanya na nani?

Dully Sykes

SOLO THANG: Nimemshirikisha Dully Sykes, niliiachia huko kisha nikarudi zangu huku.

MIKITO NUSUNUSU: Lakini kabla ya wimbo huo, ulikuwa kimya nafi kiri kwa zaidi ya mwaka Nilikuwa kimya miaka miwili), nilipatwa na msiba wa dada yangu, nilipumzika kurekodi.

MIKITO NUSUNUSU: Unakumbuka nini enzi zenu mlipokuwa wachache kwenye gemu na sasa Bongo kuna utitiri wa wasanii?

Aaah, enzi zetu hatukuwa wachache sema kutoka ilikuwa ngumu mpaka uwe na uwezo na kipaji cha kweli. Hata maprodyuza uwezo zaidi, nakumbuka kwa P-Funk ilikuwa huwezi kurekodi mpaka uwe tight and real, leo easy hata Harmorapa anatinga pale na anasifi wa na Majani! Muziki umebadilika.

MIKITO NUSUNUSU: Unafi kiri ni nini kimefanya haya yote hadi muziki uwe rahisi? Software zimefanya muziki uwe rahisi zaidi. Hata asiyeweza kuimba anaweza wezeshwa na software na ngoma ikahiti.

MIKITO NUSUNUSU: Kwa nini Uchu na Dully na si msanii mwingine Bongo?

Dully ni mkongwe na ninaheshimu kazi zake na siku zote tuna uhusiano mzuri na mawasiliano mazuri na ilikuwa hatujawahi kukaa kwenye ngoma moja. Nashukuru kaitendea haki.

MIKITO NUSUNUSU: Mlirekodia studio gani?

Mr T Touch

SOLO THANG: Kwa Mr T Touch.

MIKITO NUSUNUSU: Huko unafanya muziki au ni hadi uje huku?

SOLO THANG: Nipo Ireland, nafanya muziki kote kote, zipo studio narekodi huku na huko.

MIKITO NUSUNUSU: Una albamu ngapi hadi sasa?

SOLO THANG: Albamu ninazo nne; Homa ya Dunia, Kima cha Chini, Kilio Changu na I am Travellah. Najipinga kufanya albamu ya tano. Inayofuata inaitwa S.u.m.u

MIKITO NUSUNUSU: Nini hukipendi katika maisha yako?

SOLO THANG: Sitaki ujinga, maradhi na umaskini.

MIKITO NUSUNUSU: Una mpango wowote wa kurudi Bongo kukita makazi?

SOLO THANG: Kwa sasa sina mpango wa kuja kuweka makazi, mimi na familia yangu makazi yetu ni Dublin

MIKITO NUSUNUSU: Unamkubali msanii gani Bongo kwa sasa? Tupe Top Three yako kwa sasa

SOLO THANG: Wa aina gani ya muziki.

MIKITO NUSUNUSU: Hip Hop…

SOLO THANG: Moe Tech (Jay Mo), Prof Jay na Bill Nass.

MIKITO NUSUNUSU: Umetisha, huko wanaupokeaje muziki wako? Shoo zinalipa?

SOLO THANG: Shoo zinalipa na maisha yanaenda.

MIKITO NUSUNUSU: Una watoto wangapi so far? Ulifunga ndoa?

 SOLO THANG: Watoto ninao wann-e, nilifunga ndoa mwaka 2006.

 MIKITO NUSUNUSU: Uliwahi kuzaa na muigizaji Wastara Juma, nini unaweza kumwambia?

 SOLO THANG: Yeah tuna mtoto mmoja anaitwa Fares.

 MIKITO NUSUNUSU: Nini unaweza kumwambia?

 SOLO THANG: Kuhusu nini sasa? Nimwambie?

 MIKITO NUSUNUSU: Chochote!

SOLO THANG: Sina.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.