The House of Favourite Newspapers

Ulimwengu Amtolea Nje MO Simba

Straika, Thomas Ulimwengu

BAADA ya mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kudai alipanga kumsajili straika, Thomas Ulimwengu mwenyewe ameibuka na kusema hakuwa na mpango wa kujiunga na timu hiyo wala hata asingekubali ushawishi wake.

 

Ulimwengu amejiunga na klabu ya Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa mwaka mmoja akitoka kwenye majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwaka.

 

MO alitoa kauli ya kuashiria walikuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo baada ya straika Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga kwenye kikosi cha KRC Genk ya Ubelgiji kuweka picha ya Ulimwengu kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram na kuandika: Sinaga shaka na wewe mwanajeshi wangu kila la kheri katika makazi na majukumu mapya. MO akakomenti “Angepaswa kujiunga na Simba”.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ulimwengu alisema; “Nadhani alipenda yeye kuona inatokea hivyo kama angekuja na angeonana na mimi ni vizuri lakini sidhani kwa ukuaji wangu kisoka kama ningerudi kucheza Tanzania.”

 

“Simba ni timu kubwa na nyingine za Tanzania naziheshimu ila nimepata ofa nzuri katika nzuri kwa sababu mipango yangu bado inalenga kurudi Ulaya.

 

“Nimechagua Al Hilal kwa sababu ni timu kubwa ndiyo maana nimechagua pale kwa kuwa nitacheza mechi za kutosha, ingawa timu nyingi zilikuwa zinanitaka, zipo za kutoka Afrika Kusini ila nimechagua pale kwa kuwa ni timu kubwa,” alisema Ulimwengu ambaye ni mchezaji wa zamani wa TP Mazembe ya DR Congo.

NA IBRAHIM MUSSA

Comments are closed.