The House of Favourite Newspapers

Ulimwengu Kwisha! Aoa Mkwewe Awa Mke wa Pili

0

MWANAUME mmoja, Vvashko Sande wa Zimbabwe alishangaza kijiji chake alipoamua kuoa mkwewe na kumfanya mke wa pili.

 

Mwanamume huyo alimpenda mama mkwe wake na mapenzi yalivyozidi kunoga jamii ikagundua siri za wawili hao.

Habari zinasema kutokana na tukio hilo, mkewe alimpeleka mahakamani na kumshutumu kwa kutelekeza wajibu wake katika ndoa na kuoana mkwewe.

 

Katika mataifa karibu yote ya Afrika, uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanamume na mama mkwe huwa unaleta laana na adhabu kali ikiwemo ya kufukuzwa nyumbani.

Vvashko Sande alishangaza kijiji chake na kusababisha kuonywa na wazee na mke wake, Vimbai Magora, hata hivyo ilikuwa kama ameziba masikio.

 

Bi Magora anayesemekana kuwa na watoto wanne na Sande alishindwa kuvumilia akaamua kufungua kesi mahakamani.

Mahakamani alimshutumu mumewe kwa kutelekeza familia na wajibu katika ndoa na kumtusi kwakuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mama yake.

 

“Tulioana 2008 lakini kutoka 2011 mume wangu ametelekeza majukumu yake kwa sababu alianza uhusiano na mama yangu mzazi,” Magora alimwambia hakimu katika mahakama moja mjini Zvishavane, Zimbabwe.

 

Magora alimwambia hakimu kuwa Sande alikuwa akimpiga na kumtusi na kwamba alimtishia kumfukuza nyumbani pamoja na watoto wao wanne. “Hata adhabu ya wazee haikuweza kumfanya kuacha tabia hiyo kwani badala yake alimuoa mama yangu na kumfanya mke wa pili,” alilalamika mama huyo.

 

Akijitetea mbele ya Mahakama, mwanamume huyo alieleza mahakama kuwa aliwapenda wote wawili (mama na mwanaye) na alikuwa akitaka kukaa nao na sasa ameamua kuoa. Cha kushangaza ni kuwa mahakama ilikataa kubatilisha ndoa hiyo ya pili!

Stori: Mwandishi Wetu

Leave A Reply