The House of Favourite Newspapers

Ulimwengu: Simba Wazuri, Ila Hatuwaogopi

Thomas Ulimwengu

STRAIKA wa JS Saoura, Mtanzania Thomas Ulimwengu amefunguka kuwa kikosi cha wapinzani wao Simba ni bora kutokana na kuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa lakini hawawazidi waliopo katika kikosi chao.

 

Ulimwengu ambaye amewahi kucheza TP Mazembe ya DR Congo, leo Jumamosi ataiongoza Saoura kupambana na Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya 16 Bora, mechi ambayo itapigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Ulimwengu ambaye hii ni mara ya pili kucheza na timu za Tanzania akiwa na timu za kigeni, ameliambia Championi Jumamosi, kuwa licha ya kusikia Simba waliofanya usajili wa bilioni 1.3 kuwa ni wazuri, lakini kwao hawatajali hilo na badala yake watapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

 

“Kwanza nimefurahi kurudi kucheza nyumbani kwa mara nyingine lakini niwaambie wapinzani wetu kwamba tumejiandaa kwa ajili ya kupambana nao vilivyo. “Nasikia Simba ni wazuri lakini sisi ni wazuri kuliko wao, na niwaambie kwamba tutapambana nao uwanjani kwa ajili ya kusaka matokeo mazuri.

 

Mimi binafsi nimejipanga kwa ajili ya jambo hilo kama nikipata nafasi,” alisema Ulimwengu. Ulimwengu alijiunga JS Saoura hivi karibuni akitokea Al Hilal ya Sudan ambapo alivunja mkataba wa kuichezea licha ya kujiunga nao kwenye dirisha kubwa la usajili.

Stori na Sweetbert Lukonge na Said Ally, Dar


MCHEZAJI Anayekipiga katika klabu ya JS Saoura ya nchini Algeria Thomas Ulimwengu amesema kuwa wamejindaa vyema kuikabili Simba katika mchezo wao huo wa hatua ya makuni utakaopigwa jumamosi ya januari 12, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.