The House of Favourite Newspapers

Ulinzi Mkali Mbowe Akihojiwa na Polisi, Lowassa Azuiliwa Getini

1

ulinzi 2 ulinzi

Ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe leo  amewasili Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kuitikia wito wa kuhojiwa na jeshi hilo huku ulinzi mkali ukiwa  umeimarishwa .

Mbowe akiwa na msafara wa magari nane walikutana na ulinzi mkali ambapo magari ya Mbowe na Wakili Peter Kibatala ambaye alikuwa na Tundu Lissu ndio yaliruhusiwa kuingia.

Gari laWaziri Mkuu Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa na viongozi wengine wamezuiwa kwenye geti la kuingia kituoni hapo ambapo geti hilo limezibwa na gari la maji ya kuwasha ili kutoruhusu gari yoyote kutoka au kuingia kituoni.

1 Comment
  1. David Bupilipili says

    Ukuta

Leave A Reply